Tabaka la kati ndio lenye uwezo wa kufanya mapinduzi ya ndani wakati yanapohitajika

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
1.Tabaka tawala.
2. Tabaka la kati.
3. Tabaka la watu wa chini.

Kwa mujibu wa mwanafasafa Carl Marx, katika maandiko yake yeye na mwenzake Friederick Engel, wanaamini kuwa tabaka la kati ndio lenye uwezo wa kufanya mapinduzi ya ndani, wakati yanapohitajika.

Tabaka la kati, linaundwa hasa na watu wa kipato cha kati ambao wengi wao ni watumishi wa umma; wataalamu wa afya, walimu, wakandarasi, wanasheria, wafanya biashara wa kati, askari, waandishi nk.

Kundi hili linapoamua kuwa mashabiki wa kundi la watawala, ambao wengi wao wanaishi maisha ya ukwasi mkubwa, maisha ya paradiso, basi kundi lile la tatu yaani watu wa kipato cha chini wanabaki yatima bila watetezi.

Waandishi wasipoandika upuuzi wa watawala, wanasheria wasipokemea upuuzi wa watawala, madkatari, walimu na wakandarasi wasiposema mapungufu ya watawala katika kuboresha huduma mahali husika, wakaamua kuwa wapambe wa serikali, wakaamua kuwa wapiga debe, wapiga ngoma, wapiga filimbi, wakereketwa wa watawala, basi watawala wataendelea kuishi maisha ya mbinguni huku watu wa kipato cha chini, masikini wanaokula minyoo, wanaoishi na kunguni na panya ndani ya malango yao, hawatakuwa na mtetezi. Nao watadumu katika maisha hayo ya afadhali ya jana hadi mwisho wa dahari.

Lakini endapo tabaka la kati, litakataa kuwa vibaraka wa serikali na kufanya kuikemea, kuielekeza, kuikosoa, kuikumbusha, kuiangaliza, kuishauri na kuibeza; hapo ndipo serikali itachangamka kwa kuwa kundi hilo lina nguvu kubwa. Ndio kundi linalozalisha na kulipa kodi.

Lakini Carl Marx anaonya kwamba, endapo watu wa tabaka la kati wataacha kuwa wapambe wa serikali, wakaanza kunipinga kwa maovu yake, na ikiwa serikali ni kichwa ngumu basi hapo ni sawa na ku'commit suicide', ni sawa na kujitoa uhai. Serikali dhalimu inayoongozwa na majuha haitaki kukosolewa, kushauriwa, kubezwa, kuangalizwa, kukumbushwa nk. Haitaki fasihi. Na yanapotokea hayo wasioyataka, basi ardhi hupata kunywa damu hadi pomoni. Kucha na meno kung'olewa kwa koleo tena bila ganzi.

Kumbe haitoshi tu kwa tabaka la kati kuwa na nguvu ya kuichangamsha serikali bali pia ili nguvu hiyo ionekane ni lazima kufuta mstari unaotenganisha kifo na uhai. Katikati ya serikali katili, lazima kujiitoa. Ni kazi ambayo mabwege hawawezi kuthubutu.

Muungano wa kisoviet, chini ya Vladimir Lennin, ulifanikiwa kwa kuunganisha wafanyakazi ambao ni tabaka la kati, chini ya kauli mbiu "ALL WORKERS UNITE". Kama kuna mtu anatafuta silaha ya kuangamiza udhalimu katika taifa lake, silaha ya kwanza ni kuinganisha vyama vya wafanyakazi.

Fikiria, madaktari, walimu, wanasheria, wanafunzi wa vyuo vikuu, wakandarasi, waandishi na wataalamu wengine wakakubaliana pamoja! Kwa maslahi ya umma! Fikiria tu.
 
Ni bora kuwa mlemavu wa akili kwa kumsapoti Magu kuliko kuwa mzima kwa kumsapoti EL akiyanani sina chama lakini namkubali dawa yao
 
Ni bora kuwa mlemavu wa akili kwa kumsapoti Magu kuliko kuwa mzima kwa kumsapoti EL akiyanani sina chama lakini namkubali dawa yao
Kumbukumbu yetu itabaki kwenye maisha yetu, safari ndio kwanza inaanza
 
Back
Top Bottom