ideal safarimate
Member
- Mar 17, 2016
- 71
- 91
Naona kuna mfumo mpya kabisa wa kukabidhi fedha kutoka taasisi moja ya serikali kwenda nyingine. Badala ya utaratibu wa kawaida wa taasisi kutoa hundi za kawaida kwa mamlaka husika sasa imeanza kuzoeleka kwa taasisi moja ya serikali au hazina kuita waandishi wa habari na kukabidhi mfano wa hundi kama zile wanazotoa kampuni za simu kwa mshindi wa promosheni au bahati nasibu.Naelewa lengo la kampuni ni matangazo ya biashara kwa taasisi za serikali mantiki ni ipi? Kwa jinsi taasisi za serikali zinazofanya kazi uidhinishaji wa fedha ni zoezi la kawaida linalofanyika kila siku kama utaratibu ungekua huu naamini kama kila ambapo kuna zoezi ya kupeleka pesa kutoka taasisi moja kwenda nyingine au hazina kwenda halmashauri basi waandishi wangeweka kambi hazina na kamera zao mikononi kila siku. Nimeliona hili leo kwa mara ya pili bunge lilipokabidhi fedha kwa raisi Magufuli na pale hazina ilipopeleka fedha kwa mahakama.Nachelea kusema ni mbwembwe "stunt" zisizo na tija kwa serikali!