Taasisi za dini na umilikaji ardhi

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,381
Reaction score
17,608
Matokeo ya sensa yaliyotangazwa na Mh. Rais JK Kikwete hivi karibuni yameonyesha kuwa watanzania tuko karibu 45 mil. Hili ni ongezeko la watu 10 mil. tangu sensa ya 2002 (miaka 10 iliyopita). Hii ina maana kuwa idadi yetu inaongezeka kwa kasi lakini ardhi yetu haiongezeki hata sentimita moja. Watu hawa watahitaji ardhi ya kujenga makazi, kulima, kuchungia, kujenga shule, hospitali, kambi za majeshi, viwanda, viwanja vya michezo na shughuli mbalimbali za kijamii na maendeleo. Hivyo mipango ya namna ya kumilikishana ardhi na matumizi yake ni muhimu sana ili kizazi kijacho kiweze kuja kuambulia kupata japo sehemu ya kucheza na kuishi.

Hoja yangu ya leo ni namna taasisi za dini zinavyopora na kumiliki maeneo makubwa ya ardhi na kuyatumia katika shughuli nyingine za kibiashara na mambo mengine mbali na ibada. Ziko taasisi za kidini nchini ambazo zimepora na kuendelea kupora ardhi kubwa sana na kuifanyia shughuli ambazo si za kiibada na zisizolipa kodi. Taasisi hizi zinapata fedha kutoka nje ya nchi kwa madhumuni ya kupora ardhi nchini kwa kisingizio cha kujenga nyumba za ibada na taasisi za kidini kama hoteli, shule, vyuo, maduka, hospitali, gesti, ufugaji, kilimo, n.k. Taasisi hizi zinatumia udhaifu walionao wananchi kiuchumi, kielimu na kiutambuzi wa mambo katika kujichotea ardhi. Bahati mbaya huduma zinazotolewa na taasisi hizi ni za kibiashara zaidi kuliko huduma kwa wananchi. Mfano, ada ktk shule za taasisi za kidini ni ghali kupita shule za binafsi.

Hivi Tanzania tunajua ni asilimia ngapi ya ardhi yetu inamilikiwa na taasisi za dini? Tanzania inakusanya kodi kiasi gani kutoka taasisi hizi za kidini? Kizazi kijacho kitasema na kufanya nini kitakapokuta ardhi yao kubwa inamilikiwa na taasisi za kidini wakati wao hawana pa kujenga wala kuchezea? Hiki kitakuwa chanzo kimojawapo cha migogoro miaka ijayo!!

Taasisi za kidini zina nguvu kubwa za kiuchumi, utaalamu na maono. Zina uwezo wa kuwahamisha watu kwenye maeneo yao kwa kuwapa hela nyingi ili wao wamiliki eneo husika. Hivyo iko siku tutajikuta nusu ya ardhi yetu yote iko mikononi mwa taasisi za dini na kusababisha migogoro mikubwa kati ya taasisi hizi na wananchi, taasisi na taasisi, taasisi na serikali, n.k. Lazima kuwe na mipango ya kupanga matumizi ya ardhi kwa matumizi ya sasa na kizazi kijacho. Ukiangalia nchi kama Marekani na nyingine zilizoendelea wana reserves kubwa za ardhi zao. ndio maana kila wakati unasikia moto unaunguza misitu Marekani, maana yake wana reserve za maeneo mengi kwa matumizi ya vizazi vyao vijavyo.
 
Kumbe wanamiliki kihalali! Huna hoja ya msingi hapo! Naelewa unaowalenga, ndiyo zenu hizo, nyinyi mlikuwa wapi?
 
acha wivu wa kijinga ... uvivu wenu ndiyo unaowaponza ... jishughulisheni kwenye shughuli za maendeleo, uchumi, elimu na afya ... vinginevyo mtaendelea kubweka tuu
 
Wakati taasisi lengwa zikiwafundisha waumini wake thawabu zitokanazo na kumiliki ardhi, nyie mwafundishana thawabu zitokanazo na kuchoma na kuteketeza mali za taasisi lengwa. Tofauti ni hiyo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…