Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,432
- 73,078
Akizungumza na Wakuu wa mikoa na wilaya wapya Mtukufu Rais alisema tena kwa dhati kuwa wamemkamata mfanya biashara aliyekuwa anaiba milioni 7-8 kila dakika na kuwa keshatuibia matrilioni na kuwa yuko mikono salama sasa hivi.
Hilo ni tangazo la Rais kwa umma. Leo vyombo vinavyo husika vimesema jina la mtu huyo na kuwa ni jumla ya kama bilioni 29 ndio zimeibiwa tofauti na tangazo la matrilioni la Rais.
Kwa vile Rais ndiye akiyetangaza basi vyombo vya habari vilimsifia yeye kuwa kakamata wezi hao na mafisadi wakubwa (ingawa kiasi kina walakini na uhalisia)na kuwa hizo ni juhudi zake.
Hofu yangu ni kuwa, hayo ni makosa ya jinai na yalipaswa yatangazwe na vyombo husika kwanza kisha yeye afanye rejea katika hotuba zake kwani hizi kesi za jinai zaweza kuja kukosa ushahidi wa kutosha na serikali kushindwa na picha itakuwa Rais kashindwa kesi.
Ndio yaweza kuwa habari kama hiyo inaleta sifa kwa Rais kisiasa lakini awe makini na sifa za aina hiyo. Hatutaki kuona baadae anaaibika.
Kwanza kwa taarifa yake kuwa wizi wa milioni 7-8 kwa dakika na kuwa ni matrilioni ulishaleta taharuki lakini pia umemuaibisha mtukufu Rais wetu kuwa alitoa taarifa ya uongo.
Aachie wahusika wayatangaze wao.