Taasisi ya Manjano Foundation yawakomboa wanawake wa Zanzibar kiuchumi

RAHA KAMILI

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
203
83
[FONT="georgia" , "times new roman" , serif]
[/FONT]
[FONT="georgia" , "times new roman" , serif][FONT="georgia" , "times new roman" , serif] Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation mama Shekha Nasser .
Taaasisi ya Manjano Foundation inaendesha mafunzo ya siku 5 kwa Wanawake wa mjini Zanzibar. Taasisi hiyo inaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kumkomboa mwanamke aweze kujiongezea kipato na kukua kiuchumi.Katika mafunzo hayo yanayoendelea kwenye Hotel ya Mtoni Marine Zanzibar wanawake hao watapatiwa elimu namna ya kuanzisha na kuendesha biashara. Pia watajifunza namna ya kujiwekea akiba na kutafuta masoko na kutoa huduma bora kwa wateja wao.[/FONT][/FONT]
[FONT="georgia" , "times new roman" , serif] [/FONT]
[FONT="georgia" , "times new roman" , serif]Washiri wa mafunzo hayo..
Mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu mbili, katika awamu ya kwanza washiriki watapewa mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendesha biashara, pia kuwapa uwezo wa kutambua nafasi yao kwenye jamii wakiwa kama wanawake na kuondoa woga wa kujihusisha na kufanya kazi kwa juhudi na weledi katika biashara zao ambapo Mkufunzi wa masomo hayo ya maswala ya Biashara ni Mama Salma Salim Omar wa Zanzibar Chamber of Commarce.
[FONT="georgia" , "times new roman" , serif] [/FONT]
[/FONT]
[FONT="georgia" , "times new roman" , serif]Baadaye mtaalamu wa maswala ya urembo na matumizi ya sahihi ya vipodozi Mama Shekha Nasser atatoa ujuzi wa matumizi ya vipodozi pendwa vya LuvTouch Manjano, mfano kupamba maharusi na utunzaji wa ngozi.[/FONT]
[FONT="georgia" , "times new roman" , serif] [/FONT]
[FONT="georgia" , "times new roman" , serif]Picha ya Pamoja ya Wanawake wa Zanzibar waliojitokeza kwenye Mafunzo ya Ujasiriamlai .[/FONT]
[FONT="georgia" , "times new roman" , serif]
Mwisho wa mafunzo haya washiriki wote watakopeshwa mitaji kwa ajili ya kuanzisha na kuendesha biashara zao. Katika hatua nyingine washiriki wa mafunzo hayo waliojitokeza kwa wingi wameishukuru Taasisi ya Manjano Foundation kwa kuwakomboa na mafunzo ya kiuchumi na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.[/FONT]
 
Back
Top Bottom