Taarifa ya Uamuzi wa kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,292
15,249
68c01444a0a90d9185d3b06247f73b19.jpg

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana tarehe 23 Aprili 2017 imekamilisha mapitio ya maamuzi ya Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Masaa 72).

Baaada ya Mapitio hayo yafuatayo yamejitokeza :

I. Kamati kwa kauli moja imeona kuna Kasoro za kikanuni katika maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji wa Usimamizi wa Ligi kwa sababu zifuatazo:

1.Malalamiko ya Klabu ya Simba kutowasilishwa kwa wakati kwa mujibu wa kanuni 20(1) ya Kanuni za Ligi Kuu toleo la 2016 inayotaka malalamiko yoyote yanayohusiana na mchezo yawasilishwe kwa maandishi Bodi ya Ligi Kuu sio zaidi ya masaa 72 baada ya mchezo kumalizika.

2.Malalamiko hayo hayakulipiwa ada kwa mujibu wa kanuni 20(4) kinachosema ada ya malalamiko ni Shs. 300,000/= (Shilingi laki tatu). Malalamiko yatakayowasilishwa bila kulipiwa ada au baada ya muda uliowekwa hayatasikilizwa.

3.Kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa ligi kilikosa uhalali baada ya kuwashirikisha wajumbe waalikwa ambao sio sehemu ya kamati hiyo.

Hivyo kwa msingi huo malalamiko ya Simba hayana mashiko kikanuni hivyo matoko ya mchezo wa Kagera Sugar dhidi ya Simba Sports Club yanabakia kama yalivyokuwa awali (2-1).

Pia kamati kwa kupitia taarifa za mchezo namba 165 unaolalamikiwa wa Kagera Vs Africa Lyon kumejitokeza mapungufu mengi ya msingi kwa mujibu wa rekodi zilizopokelewa na Bodi ya Ligi na kutumika katika kikao tajwa, kwa mfano:

1- Matokeo ya mchezo referee na kamisaa walipishana,mmoja (Kamisaa) alisema matokeo ya mwisho wa mchezo yalikuwa 2-1 na Mwamuzi alisema 2-0.

2- Refa na Kamisaa wanapishana sababu ya adhabu hiyo mwamuzi anasema kumvuta mpinzani na Kamisaa anasema kumrukia mpinzani.

3- Kamisaa kutopeleka taarifa ya mchezo TFF kwa maelezo ya kukosea address ya barua pepe kwa mara ya kwanza toka awe kamisaa.

4- Bodi ya Ligi kutumia matokeo ya Kamisaa yaani 2-1, na kwa msingi huo taarifa ya refa kukosa weledi. Uzoefu unaonyesha ni rahisi kukumbuka matokeo sio kadi.

5- Utoaji taarifa wa refa kupitia address ya barua pepe ya mtu mwingine kwa maelezo yanayo pelekea kutia shaka weledi wake kuwa alipoteza simu na hivyo mabadiliko ya simu ndiyo kiini cha utumaji taarifa kupitia barua pepe ya muamuzi mwenzake kinyume na utaratibu.

6- Kutofanyika kwa kikao cha brief ya waamuzi baada ya mchezo kama ilivyo ada kwa maelezo ya mwamuzi kuwa hakukuwa na tukio.

7- Uongozi wa African Lyon kugoma kutoa ushirikiano kwa kamati juu uwepo wa kadi ya njano kwa sababu za kuogopa kuathiriwa na ushiriki wao katika suala hili.

8- Mchezo kubadilishwa tarehe na hivyo kukosekana records.

9- Ligi kusimama baada ya mchezo wa Kagera Vs Majimaji toka tarehe 4.3.2017 Mpaka tarehe 2.4.2017 ambapo Simba ilicheza na Kagera na kwa hivyo kulikuwa na muda wa kutosha kwa chombo kinachosimamia ligi kuweka rekodi sawa kupitia mfumo wa taarifa.

10-Uwepo wa rekodi zinazoonyesha maamuzi ya refa kuhusu utoaji wa kadi sio ya mwisho.

Yote hayo hapo juu yanazua maswali juu ya uwepo wa taarifa sahihi za kadi na hivyo kufanya hoja pinzani yaani BENEFIT OF DOUBT iwe IN FAVOR OF KAGERA SUGAR FC.Kwa kuwa ni rahisi kukumbuka matokeo na sio kadi.

Vilevile Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imependekeza kupitia kwa ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF:

1- Kuwachukulia hatua stahiki watendaji na maofisa wote ambao ama hawakuwajibika ipasavyo au kutenda kosa la kuipotosha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi kinyume na katiba.

2- Kutoa waraka kwa waamuzi na makamisaa utakaolekeza bayana namna ya kuwasilisha taarifa kwa Bodi ya Ligi na TFF.
 
kali kuliko zote :

1- Matokeo ya mchezo referee na kamisaa walipishana,mmoja (Kamisaa) alisema matokeo ya mwisho wa mchezo yalikuwa 2-1 na Mwamuzi alisema 2-0.
 
kali kuliko zote :

1- Matokeo ya mchezo referee na kamisaa walipishana,mmoja (Kamisaa) alisema matokeo ya mwisho wa mchezo yalikuwa 2-1 na Mwamuzi alisema 2-0.

Mtu kama huyu anatakiwa afungiwe kabisa! Haiwezekani uwezo wake ukawa chini mno kiasi hiki.

Halafu anataka kuwadanganya watu kwamba uwezo wa kukumbuka matokeo hakuwa nao, ila wa kukumbuka Kadi za njano alikuwa nao.
 
Mwamuzi ameshindwa kukumbuka Matokea ya mchezo husika lakini iweje aweze kukumbuka Kadi ya njano?
Kamati ya ligi, kamati ya saa 72, kamati ya waamuzi hao wote ni maofisa wa TFF. kama wana mapungufu maana yake TFF nzima imepungukiwa weledi. kama simba walitaka kutumia rushwa ili kupata point za bure kinyume cha taratibu, TFF wachukue hatua waache porojo. haya mambo ya rushwa ambayo yanachekelewa kwenye corido za shirkisho hilo ndiyo yanayodumaza mchezo wetu tunaoupenda
 
Sababu zilizoinyima Polisi kwenye rufaa dhidi ya Simba kwenye Kombe la Shirikisho ndiyo hizo hizo zimetumika kwa Simba
Mpira ni uwanjani
 
Kumbe ndio zao hao wapolipoli!! Basi naamini hata mbao hawakuzikata wenyewe walisaidiwa tu hawa.
Halafu wanataka eti kuwakilisha bongo mashindani ya kimataifa!! Mchangani tu mnashindwa kimataifa mtaweza wapi nyinyi.
Mvumilie tu muendelee kuwa watazamaji we mechi za kimataifa.
Kama anzisheni mashindano ya kuogelea mto msimbazi mjiliwaze tu, maana hakuna namna nyingine.
 
Hata uamuzi wa Kamati una mapungufu makubwa sana;

1. Badala ya ku-establish facts, jamaa ana kadi au hana, wao wanatuletea habari ya matokeo!
Nani aliulizia issue ya matokeo.
2. Badala ya kutueleza kama uchunguzi uanonesha Fakhi alikuwa na kadi 2 au 3 (idadi) wao wametuletea sababu iliyosababisha akapata. Eti wanasema ripoti moja inasema alipewa kadi kwa kosa la kumvuta mchezaji mwenzake, mwingine akasema ni kwa kumrukia mwenzie. Sasa utata hapo ni sababu ya kadi au uwepo wa kadi?
3. Badala ya kuchunguza na kuestablish facts, wao wanatoa uamuzi kwa kuangalia benefit of doubt!
4. Badala ya kutueleza usahihi wa taarifa na takwimu za maafisa waliosimamia mchezo, wao wametueleza taarifa zilitumwa kwa email, mara binafsi, mara simu ilipotea, so what?

Ndio maana tunasema Malinzi, na TFF yake pamoja na kamati wamepoteza kabisa legitimacy ya usimamizi wa mpira. Waamuzi na Kamisaa hawaelewani, Kamati kwa kamati zinakuja na uamuzi tofauti kwenye jambo moja, and so forth.
 
Kuestablish facts
Kuestablish facts
Kuestablish facts
Kuestablish facts
Kuestablish facts

Mkuu mbona uzi unajitoshelezha huo!

Uchunguzi unaonyesha jamaa hana kadi. Inakuwaje mtu ambaye anashindwa kukumbuka matokeo ya mechi akakumbuka Kadi?

Taarifa ya mwamuzi anayesema matokeo ni 2-0 huwezi kuiamini wakati matokeo halisi yalikuwa ni 2-1.
 
Naona umekwenda haraka sana kujibu. Ni wapi waliposema jamaa hana kadi?
Au unaongeza wewe taarifa? Kwa nini mwamuzi alisema matokeo ni 2-0, badala ya hayo mnayoita ni halisi ya 2-1. Je ni typing error? Ni uzembe?. Na je haya matokeo halisi, huu uhalisi umetokana na taarifa ya nani? Kwa nini huyo aliyetoa matokeo halisi hajatupatia na uhalisia wa kadi ya Fakhi?

Vyovyote iwavyo ukikosea tarakimu kwenye kipengele kimoja, lazima ukosee na kingine?

After all kukosewa kwa ripoti ya mwamuzi kwenye matokeo kunahalalisha vipi Fakhi kuwa na kadi au kutokuwa nayo?
Halafu mbona hiyo kamati inazungumzia matokeo, hili lilikuwa ni jambo linalobishaniwa?

Haya kamati hii inazungumzia aina ya kosa lilipolekea Fakhi kupata kadi ya njano. Kuna tofauti yoyote kati ya kadi ilipotikana kwa kumvuta mtu au kumrukia?
 
Benefit of a doubt. Napendaga terminology za kisheria...Beyond any reasonable doubt!
Prosecutors bear the burden of proof and is required to prove their version of events to this standard. This means that the proposition being presented by the prosecution must be proven to the extent that there could be no "reasonable doubt" in the mind of a "reasonable person" that the defendant is guilty. There can still be a doubt, but only to the extent that it would not affect a reasonable person's belief regarding whether or not the defendant is guilty. Beyond "the shadow of a doubt"
 
Naona umekwenda haraka sana kujibu. Ni wapi waliposema jamaa hana kadi?
Au unaongeza wewe taarifa? Kwa nini mwamuzi alisema matokeo ni 2-0, badala ya hayo mnayoita ni halisi ya 2-1. Je ni typing error? Ni uzembe?. Na je haya matokeo halisi, huu uhalisi umetokana na taarifa ya nani? Kwa nini huyo aliyetoa matokeo halisi hajatupatia na uhalisia wa kadi ya Fakhi?

Mkuu.

Mimi ni mhaya na ni mkaazi wa Kagera sikuona hiana kushindwa kuangalia ile mechi.. Kwa kuwa uwanjani na kwangu ni karibu.

Unataka kusema hata mimi siyajui matokeo?

Au nikiletewa ripoti na Kamisaa na mwamuzi nitaiaini ile ya mwamuzi?

Kila mtu anajua ile game iliisha 2-1. Iweje huanze kuondoa uhalali wa ripoti ya Kamisaa!
 
Vyovyote iwavyo ukikosea tarakimu kwenye kipengele kimoja, lazima ukosee na kingine?

Pengine unaweza kupata shida kuamini, lakini mpala dakika ya mwisho Mwamuzi alikuwa anaitetea ripoti yake na kuwa hakuna kipengele kilicho kosewa! (matokeo ya 2-0 yakiwemo)

Hapo ndipo shaka ilipojitokeza ikiwa kila mtu anajua kuwa game iliisha kwa matokeo ya 2-1. Je unaanzaje kuamini hiyo ripoti?
 
All in all awe alikuwa na kadi au hakuwa nayo yafuatayo yanabatilisha uamuzi wa kamati ya masaa 72.Makosa ya kikanuni

1.Malalamiko ya Klabu ya Simba kutowasilishwa kwa wakati kwa mujibu wa kanuni 20(1) ya Kanuni za Ligi Kuu toleo la 2016 inayotaka malalamiko yoyote yanayohusiana na mchezo yawasilishwe kwa maandishi Bodi ya Ligi Kuu sio zaidi ya masaa 72 baada ya mchezo kumalizika.

2.Malalamiko hayo hayakulipiwa ada kwa mujibu wa kanuni 20(4) kinachosema ada ya malalamiko ni Shs. 300,000/= (Shilingi laki tatu). Malalamiko yatakayowasilishwa bila kulipiwa ada au baada ya muda uliowekwa hayatasikilizwa.

3.Kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa ligi kilikosa uhalali baada ya kuwashirikisha wajumbe waalikwa ambao sio sehemu ya kamati hiyo.
 
Kuestablish facts
Kuestablish facts
Kuestablish facts
Kuestablish facts
Kuestablish facts

Mkuu mbona uzi unajitoshelezha huo!

Uchunguzi unaonyesha jamaa hana kadi. Inakuwaje mtu ambaye anashindwa kukumbuka matokeo ya mechi akakumbuka Kadi?

Taarifa ya mwamuzi anayesema matokeo ni 2-0 huwezi kuiamini wakati matokeo halisi yalikuwa ni 2-1.
Kama Hana kadi kwanini wamemsimamisha kucheza game moja?
 
Back
Top Bottom