JUMATATU 09 JANUARI 2017.
Mheshimiwa Mgeni Rasmi Balozi Seif Ali Iddi. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (MCC)
Mheshimwa Sadifa Juma Khamis. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa.
Ndugu Vuai Ali Vuai. Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Mheshimwa Mboni Muhita. Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa,
Mheshimiwa Mama Asha Balozi Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Ndugu Wajumbe wa Kamati kuu ya CCM na Halmashauri kuu ya CCM Taifa mliopo.
Waheshimiwa Mawaziri, wajumbe wa Baraza la Wawakili, wabunge.
Ndugu Wenyeviti wa CCM wa Mikoa.
Viongozi wa ngazi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake.
Wananchi, vijana wenzangu
Mabibi na mabwana.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Mgeni rasmi.
Kutimia kwa miaka 53 tokea yalipofanyika Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, 1964 si jambo jepesi na rahisi kwa vile haukuwa mpango au jambo dogo kama baadhi ya watu wanavyoweza kulichukulikia leo hii.
Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni kilele cha kumaliza ukoloni wakisultani lakini pia yalizika zama za maonevu, ukandamizaji wa haki, dhulma na kukomeshwa kwa manyanyaso dhidi ya wananchi waliotumikishwa na kuuzwa utumwani kwa karne nyingi zilizopita.
Kuingia kwa waarabu toka Oman mwaka 1832, ulikuwa ndiyo mwanzo wa manyanyaso, maonevu, ubaguzi na ukandamizaji wa haki kuliko waandama waafrika wenyeji wa visiwa vya Zanzibar.
Huduma muhimu zilitolewa kwa matabaka warabu wazungu wakiwa daraja la kwanza, wahindi na wangazija daraja la pili, na wazalendo wenyeji daraja la mwisho.
Waafrika wenyeji walinyimwa haki na fursa muhimu za kibinadamu, walikosa elimu,huduma za kiafya, maji kunywa wakiokota, wakiishi katika vibanda vya matope na maakazi duni.
Katika utawala wa kisultan wakishirikiana na wakoloni wenzao wa kiingereza katika kuikalia Zanzibar kimabavu, waafrika wenyeji wa Zanzibar walibaguliwa na walinyanyaswa huku wageni warabu kutoka Oman wakifurahia maisha mazuri wao na mabwanyenye wenzao.
Mheshimiwa mgeni rasmi.
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunayazungumza haya ili kuwakumbusha na kuwatanabahisha vijana wenzetu ambao mara kadhaa huingia katika majaribu ya kudanganywa na Hizbu Matope waliobakia huku wakificha ukweli na kutojua wapi wazee wetu wametoka, taabu, dhiki na dhoruba walizozipata kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar 1964.
Wakati kila mwaka tukiendelea kufanya matembezi haya sisi vijana wa Chama Cha Mapinduzi tumekuwa ni mashahidi wa kujionea jinsi gani ambavyo baada ya miaka 53 ya Mapinduzi watu wakiishi bila kubaguana, kutengana aidha kwa nasaba, rangi, Kabila au asili yao, hayo ni miongoni mwa matunda ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yaliotandikwa kwa zulia la usawa, haki na kujenga umoja wa kitaifa.
Mheshimiwa Mgeni rasmi
Wakati Zanzibar ikifikisha miaka 53 tokea kufanyika Mapinduzi Januari 12, 1964 bado Vijana kwetu ni jambo gumu na lisilowezekana kabisa kuzungumzia mafanikio ya Mapinduzi hayo bila ya kuwahusisha au kuwataja wanamapinduzi 14 vijana wa mstari wa mbele ambao waliojitolea muhanga hadi kuuangusha utawala wa kisultan.
Vijana hao wa Chama Afro Shiraz Party (ASP) waliongozwa na Jemedari Mkuu Hayati Sheikh Abeid Amani Karume: Seif Bakari Omar, John Gedion Okello, Abdallah Said Natepe, Khamis Daruwesh, Abdallah Kaujore, Yussuf Himid Maftah, Pili Khamis Mpera, Hamid Ameir Ali, Said Washoto, Said Idd Bavuai, Hafidh Suleiman, Abdallah Mfaranyaki na Khamis Hemed Nyuni Mwenyezi Mungu awarehemu na awalaze mahali pema pepo na Brigedia mstaafu Ramadhan Haji Faki Mwenyezi Mungu ampe umri mrefu na afya njema.
Mheshimiwa Mgeni rasmi
Wakati tukiadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi, Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunaendelea kuamini kuwa bila ya ujasiri, ushupavu, ukakamavu, uzalendo na uthubutu wa Vijana hao hadi sasa utawala wa kisultan ungalikuwa ukiendelea kuvikalia visiwa vyetu kwa kivuli geresha cha Waingereza kuipatia uhuru bandia Zanzibar Disemba 10, 1963 na wao kuamua kuondoka huku wakimwacha Sultan akiwa amebaki juu ya kiti chake.
Hivyo sisi Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunahidi mbele yako kuwa Vijana hawa 14 hawatasahaulika, bali tutaendelea kuwakumbuka, kuwaenzi na kuthamini milele mchango wao walioutoa kwa Taifa letu.
Ni kovu lisilopona kwa kila mzalendo wa Taifa hili kila akikumbuka jinsi wazazi wetu huko nyuma walivyoteswa sana chini ya utawala wa sultan, walinyanyasika na kuishi kwa mateso makali hadi pale ukombozi kamili ulipopatikana Januari 12,1964 .
Wakati wote tulipokuwa tukitembea na kupita katika maeneo mbali mbali ya viunga vya miji na vijiji tulijitahidi kupaza sauti zetu ili kuwakumbusha wananchi hususan Vijana wenzetu wasikubali kudanganyika, wakatae kughilibiwa na wasaka madaraka wasio na uchungu wala hisia za wapi tulikotoka na tulipo leo.
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tumetembea kuidhihirishia dunia na kila mmoja ajue kuwa Mapinduzi haya yalifanywa na vijana wenzetu kama sisi kwa wakati ule. Kazi yao wameikamilisha ipasavyo, tena kwa uhakika na uzalendo na kufanikiwa kuuangusha utawala wa kisultan madarakani.
Kazi yetu sisi vijana wa kizazi hiki si kufanya tena Mapinduzi mengine, hivyo tunatambua kuwa wajibu na jukumu letu ni kuhakikisha Mapinduzi tulioachiwa na wenzetu yanalindwa, yanathaminiwa na misingi yake inaendelezwa ipasavyo hatua kwa hatua bila kudhofishwa.
Mhe Mgeni rasimi
Wakati huu tukiadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi bado vyama vya upizani wana ndoto ya kuitoa CCM madarakani hawa tunawafananisha na mgonjwa wa akili anaishi hospital Kidongochekundu aliyamua kujipmba kama bi harusi akitangaza harusi lakini waliomjuwa kuwa anatoka hospital ya wagonjwa akili walibakia kucheka. CCM katika kuyalinda Mpinduzi na Muungano itaendelea kuongoza dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar. Kwa dhamira ile ile ya kuwakomboa wazalendo waafrika wa Tanzania.
Vijana 400 tuliotembea katika matembezi haya tumebeba kauli mbiu hii ya ASIYE YAENZI MAPINDUZI NI ADUI WA MAENDELEO YA ZANZIBAR ni imani yetu ujumbe kwa wote popote pale walipo.
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wakati wote tukitembea tumekuwa tukikumbuka, kutaka kujua, na kujiuliiza hatimaye tupate majawabu kwanini wazee wetu walifikia uamuzi wa kusema heri ya kufa kuliko kutawaliwa.
Tunaendelea kuamini kadri ya tunavyopata uwelewa na ufahamu ndivyo mapinduzi yetu yatakavyoendelea kudumu ili kusitokee kidudu mtu kutania au kuhatarisha uwepo wake.
Umoja wa Vijana wa CCM tumelazimika kuyakumbusha hayo kwa hisia na uchungu na kuamua kila mwaka kufanya matembezi haya ya hiari na amani, kukumbuka na kuenzi mchango na nguvu zilizotolewa na wazee wetu waliomua kufanya Mapinduzi.
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tutaendelea kusema kweli daima mahali popote pale tutakapoona hiki na kile hakifanyiki kwa kuzingatia misingi ya Mapinduzi kadri ilivyoelezwa na tutakosoa bila ya kuwa na mbegu za unafiki kwa vile unafiki nao ukimea huwa ni saratani.
Mheshimiwa Mgeni rasmi.
Itakumbukwa kuwa sasa ni takriban miaka 5 mfululizo matembezi haya yamekuwa yakifanyika ambayo yameongeza ari na hamasa kwa vijana wa Chama Cha Mapinduzi katika kuyalinda kwa vitendo Mapinduzi yetu.
Mheshimiwa Mgeni rasmi.
Umoja wa Vijana wa CCM unatoa shukrani nyingi na za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein kwa michango, ushauri na maelekezo.
Katika kipindi chote matembezi haya yakifanyika Dk Shein amekuwa mlenzi mzuri na kinara wa kuhakikisha Umoja wa Vijana unasonga mbele na kuimarika siku hadi siku, Aidha tunakushukuru wewe binafsi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, leo hii hatuna la kusema zaidi Ahsante kwa yote mema unayotutendea vijana wako.
Mwisho kwa niaba ya vijana wote tunamshukuru sana Mwenyekiti wetu Mheshimiwa Sadifa Juma Khamis kwa usimamizi na uongozi bora katika taasisi yetu, kudumu kwa matembezi haya miaka 5 mfululizo ya uongozi wake ni kilelezo na alama isiyofutika ndani ya jumuiya, chama na Taifa letu.