Teh mkuu naona unatka kumharibia MUKULU siku yake aisee........Namwamini Mzee Mwanakijiji kuliko hata Kikwete, he is better than Kikwete upstairs. Kudos brother
Hahahahaa....na mimi nasema apigwe tu.Mzee Mwanakijiji apigwe tu maana tumechoka na hatuna njia nyingine..
Simu ya Upepo : "N G O M E" Makao Makuu ya Jeshi,JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES SALAAM,12Septemba, 2013.
Tele Fax : 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limepata habari kupitia mtandao wa Jamii Forum na Gumzo la Jiji na mingineyo kuwa likizo zimesitishwa Jeshini na waliokuwa likizo wameitwa kurudi kazini.Taarifa kwa vyombo vya Habari
Taarifa hizo pia zimeeleza kwamba Brigedi za Tembo na Kifaru zimepewa maagizo ya kuwa katika hali ya utayari endapo watahitajika kusonga mbele.
JWTZ linapenda kuwaeleza wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa taarifa hizo ni za upotoshaji mtupu na hazina ukweli wowote. Aidha, taarifa hizo ni zenye nia ya kuzorotesha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yetu (Tanzania) na majirani zake.
Sambamba na taarifa hii, pia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa za kutohusika na viunganishi vya JWTZ kwenye mitandao ya ‘Facebook‘ – (Facebook/JWTZ) na ‘Twitter‘ (Twitter/ JWTZ).Mitandao hiyo yenye viunganishi vya JWTZ imekuwa ikijihusisha na kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikichangiwa na watu mbalimbali, ambapo baadhi yao wamekuwa wakitoa taarifa za upotoshaji na zisizo sahihi. Tunapenda kutaarifu kwamba akaunti za facebook na twitter zilizotajwa siyo za JWTZ.Hatua zimechukuliwa za kuwatambua wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria.
Aidha inasisitizwa kwamba JWTZ lina taratibu za zake zinazotumika kufanya mawasiliano na Vyombo vya Habari, Taasisi, au mtu binafsi kuhusu utoaji wa taarifa.Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi
Dar es salaam, Tanzania
Watawachukulia hatua jf? Nijuavyo mimi jf=Watanzania, hii ina maana kua habari zinazopatikana jf huandikwa na wanachama wa jf ambao wengi wao ni Watanzania. Sidhani kama wasimamizi wa jf huwatuma watu kuandika habari yeyote, wao kazi yao ni kuchuja habari kama ni za ukweli ama za uzushi na kuzifuta.
Kwa mtazamo huu jwtz wanataka kupambana na Watanzania, sawa tusubiri ila wakati wanafanya hivyo wasisahau kusoma "disclaimer" ya jf waone inasemaje ndipo waje na mikakati yao.
Wadau nawasalimu woote,,
Leo asbh kupitia vpindi vya MAGAZETI redioni zimeskika habari kuwa Jeshi la Wanachi Tz limetangaza mgogoro usiokoma kati yake na mitandao ya kijamii ikiwemo JF kwa kile kibachodaiwa kuwa Wamepakaza habari za uwongo kuwa Likizo zoote kwa Wanajeshi zimefutwa na wanajesh walokuwa likizo kurejeshwa makazini mara moja kufuatia hali ya hatari iliyokuwa imetanda nchini, JWTZ imedai kuwa habari hizo ni za kipotoshaji na uongo mkubwa na serikali haitasita kuwachukulia hayua wahusila.
Anaejua undani wa hili afunguke hapa
Hiyo email address ya JWTZ ni kichekesho namba moja.
Kichekesho namba mbili ni hiyo website.....HAIPO.
Mleta uzi na gazeti lako mnatuchanganya..
Mbona hii taarifa haioneshi kuilaumu JF au kuichukulia hatua yoyote??
Hahahahaa....na mimi nasema apigwe tu.
Sawa nimekuelewa kwamba inawezekana kupata IP address kwa kadri inavyotakikana. Na kwa mwendo wa humu jf tutasombwa wengi sana.
Ndiyo hawa jamaa katika zama hizi, kwenye maazimisho ya sherehe zao huwa wanavunja mawe na matofali kwa vichwa?