Taarifa kwa wale walioappeal mikopo elimu ya juu

nyakandula

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
1,244
1,718
TAARIFA KWA WALE WALIOAPPEAL MIKOPO

Ndugu waheshimiwa viongozi,kufuatia uhakiki unaoendelea ktk bodi ya mikopo kuhusiana na wanafunzi walioappeal yafuatayo yamebainika.

1.Baadhi ya wanafunzi walituma fomu zao za appeal bila hakimu kusaini na kugonga muhuri.

2.kuna wanafunzi wamebadili index number yaani kwa mfano wengine awali walitumia index number za form iv ktk kuomba Mkopo lakini wakati wa kuappeal wametumia index no ya vi.

ili kuweza kuondoa changamoto hiyo ninaomba viongozi wa Wanafunzi vyuo vyote fanyeni yafuatayo kabla ya kufungwa kwa zoezi la kupokea fomu mnamo
30/01/2017.
1.Shirikianeni na Wanafunzi pamoja na uongozi wa Chuo kuhakikisha Wanafunzi hao wanasaini fomu zao kwa hakimu na kwa Dean of students kisha kuandikiwa barua na uongozi wa Chuo inayoelezea sababu za kutumwa upya fomu hizo bodi ya mikopo.

2. Wasisitizeni Wanafunzi wote walioappeal mikopo waandike barua za kutambulisha index number zao za form four na form six,na waziambatanishe katika form zao za appeal.kwa kufanya hivyo itasaidia sana kuondoa mkanganyiko wa index no uliopo bodi ya mikopo.

3.Hakikisheni fomu hizo zinakamilika mapema na kutumwa bodi ya mikopo kabla ya 30/01/2017.

Mwisho ninawaomba sana waheshimiwa viongozi kila mtu katika eneo lake atimize wajibu wake kikamilifu kwa kuhakikisha zoezi hili linakamilika ndani ya wakati ili tuweze kufuatilia Wanafunzi wenye sifa wapate mikopo.
Thomas M.Amos
KAMISHNA IDARA YA MIKOPO NA UDAHILI
 
Back
Top Bottom