Taarifa kwa Umma: Serikali yakanusha kuhusu uvumi wa ajira mpya za walimu

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
TAARIFA KWA UMMA
Kumekuwa na taarifa za upotoshaji zinasombazwa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kutolewa kwa ajira mpya ya walimu kwa shule za sekondari na msingi kwa mwaka 2015/2016.

Taarifa hizo zinazosambazwa zinaeleza kwamba walimu wapatao 17,928 wa cheti (Daraja IIIA) , 5,416 wa Stashahada kwa sekondari na 12,677 kwa shule za mazoezi za vyuo vya ualimu Tanzania Bara wamepangwa kwa ajili ya kuanza kazi.

Katika taarifa hiyo inawataka walimu hao waliopangwa kuripoti kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kupangiwa vituo vya kazi na kuanza kazi tarehe 01/04/2016.

Taarifa hizo pia zinaeleza kuwa walimu ambao hawataripoti ifikapo tarehe 10/04/2016 hawatapokelewa tena na watakuwa wamepoteza ajira zao.

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inapenda kuchukua nafasi hii kukanusha taarifa hizo kuwa ni za upotoshaji. Wananchi wanapaswa kuzipuuzia kwani mpaka sasa bado Serikali haijatoa ajira za walimu kwa mwaka 2015/2016.

Ajira mpya za ualimu zitakapokuwa tayari zitatangazwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari na katika tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz.

Imetolewa na :
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
11/03/2016​
 
Vijana wanalilia ajira, Elimu yetu imetutengeneza kuwa job seekers zaidi na sio job creators
 
Ajira za ualimu ni rahisi kuliko ajira zingine..hazina interview wala uzoefu kazni
 
Hivi walimu wanaoomba ajira na wanaosubiri kuajiriwa wako serious kwenda kufanya Kazi hii au wanataka tu ajira?
 
Back
Top Bottom