Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) kinawaalika na kuwakaribisha Wazanzibari na Wananchi wote kwa ujumla katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kesho, Jumamosi tarehe 21 Januari, 2017 katika uwanja wa mpira wa Dimani kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni.
Mkutano huo wa kufunga kampeni kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani utaongozwa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akiambatana na Mgeni Maalum wa Mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Aikael Mbowe.
Pamoja na Viongozi hao, Mkutano huo utawajumuisha viongozi mbali mbali wa kitaifa,akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Mh. Nassor Ahmed Mazrui, Makamo Mwenyekiti mstaafu wa CUF Mh. Juma Duni Hajj, Wakurugenzi wa Chama Taifa kama vile Mh. Omar Ali Shehe na Mh. Ismail Jussa Ladhu.
Viongozi wengine watakaohudhuria mkutano huo ni Wajumbe wa Baraza kuu la Uongozi la Taifa la CUF kama vile Mh. Abubakar Khamis Bakar, Mh. Said Ali Mbarouk, Mshauri wa Mikakati wa Katibu Mkuu wa CUF, Mh. Mansour Yussuf Himid na viongozi mbalimbali kutoka Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Imetolewa na:
Hissham Abdukadir
Afisa Habari na Mawasiliano
CUF-Makao Makuu
Zanzibar.