Taadhari : Epuka kampuni hii ya kitapeli!

Taadhari : Epuka kampuni hii ya kitapeli!

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,365
Reaction score
27,754
SOCIAL Company inayojinasibu kutoa
mikopo nafuu isiyokuwa na riba kupitia
mfuko wake maalum ujulikanao kama
Social Credit & Loans, imegundulika
kuwa ya kitapeli. Kampuni hiyo imekuwa ikitumia majina
ya watu maarufu kama vile Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri, Absalom
Kibanda na mwanamuziki Judith
Wambura ‘Lady Jaydee’ ikielezwa
kwamba ni miongoni mwa wale waliofaidika na mikopo hiyo. Kwa nyakati tofauti wawili hao walikana
kuwa miongoni mwa watu waliowahi
kufaidika au kuomba mkopo kutoka
kwenye kampuni hiyo. Kampuni hiyo ambayo tayari
imewatapeli watu mbalimbali nchini,
imekuwa ikizama zaidi kufanya utapeli
huo kwa kutumia njia ya mtandao
ambako huwataka wateja wao kujiunga
kwa kupitia tovuti. Katika ukurasa wa tovuti ya kampuni
hiyo, wateja kabla ya kujisajili hutakiwa
kutoa kwanza sh. 84,000 kama ada ya
ushirika ambayo inatakiwa kuingizwa
kwenye akaunti ya M-Pesa na TIGO-Pesa
ili waweze kuwa na sifa ya kukopeshwa fedha kuanzia sh. 200,000 hadi
10,000,000 kwa muda wa dakika 45
baada ya kujiandikisha. Wanaelezea kwamba baada ya mteja
kujaza fomu hiyo na kulipia ada yake,
fomu yake itapokelewa na bodi kuu ya
utoaji mikopo, pia malipo yake
yatapokelewa na mhasibu na baada ya
hapo maombi yake yataidhinishwa na atapatiwa mkopo wake usiokuwa na
riba. Kwamba sababu za kutoa mikopo bila
riba kwa kupitia mfuko wao maalum wa
Social Credit & Loans inachangiwa na
faida wanazozipata kutoka kwenye
kampuni za simu pindi mteja anapojaza
fomu na kulipia ada kwa njia ya mitandao hiyo. Kampuni hiyo inayoonyesha kwamba
imepata usajili kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) na kupewa TIN
namba 203-334-6789 ikiwa na usajili
namba TRA. 33/SCC/REG.7894,
imeanzishwa tangu mwaka 2003 ikiwa kama tawi zawa lisilojitegemea na ni
kampuni binafsi iliyoingia ubia na Benki
ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa
makubaliano ya mikataba ya muda. Imeeleza kuwa baada ya Social Credit
Company kumaliza mkataba wake rasmi
na NBC, kwa sasa wameanza
kujitegemea na kuunda mfuko huo wa
Social Credit & Loans kwa ajili ya kutoa
mikopo. Tanzania Daima lilifika katika ofisi za
kampuni hiyo zilizopo eneo la
Kigamboni, Mji Mwema, lakini mlinzi wa
jengo hilo alisema kuwa wamiliki wa
ofisi hiyo hawafiki mara kwa mara. Msemaji wa Vodacom, Salum Mwalimu,
alikana kampuni yao kujihusisha na
utoaji wa mikopo. Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa
Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo
alikana kampuni hiyo kutambuliwa. Kayombo alisema kuwa amejiridhisha
baada ya kuifuatilia kampuni hiyo katika
mfumo wa kompyuta wa TRA, na
kwamba wameshindwa kuitambua
namba iliyotajwa kwenye fomu F-TSD
002-B. Aliongeza kuwa wamegundua kwamba
kuna tatizo katika mfumo wa TIN wa
TRA unaoruhusu tarakimu tisa, wakati
ile iliyotumika katika kampuni hiyo ina
tarakimu kumi na pia ameshindwa
kumtambua mhusika anayetumia jina la ‘Social Company.


Source : Tanzania Daima
 
asante mkuu kwa kutupa taarifa wasije wengine wakaingia choo cha kike
 
asante hili shamba la bibi mrithi ataamka lini sijui
 
Watapata wateja tu. Hivi hamjagundua Dar wajinga ni wengi kuliko werevu kwa sababu ya tamaa. Mjinga anaona akitoa 84,000 atapata 200,000 halafu ataingia mitini. kumbe akishatoa 84, 000 hatakaa aone mtu
 
Hawa jamaa mwaka jana walijiita Loan Foundation na taarifa zao zilionesha kuwa walikuwa chini ya Zitto Kabwe Foundation ambaye naye alikana kuhusika.
Taarifa yao iliongeza kuwa "powered by tigo". Nilifanya juhudi za kwenda ofisi za tigo nao walikana kuhusika ila walikiri baadhi ya wateja kwenda kulalamika kwao.
Cha ajabu na cha kushangaza ambacho nilikipata pale ofisi za tigo, nikaambiwa wamezifunga zile tigopesa acc ili wasiweze kutoa pesa, lakini kila ilipofika dk 15 pesa ziliyeyuka na kuondoka mtandaoni. Kwa maana kwamba zilikuwa zinatolewa.
Nikabaki na baadhi ya maswali kwamba labda watu wa IT ndani ya kampuni za simu wanahusika na utapeli huo.
 
Watapata wateja tu. Hivi hamjagundua Dar wajinga ni wengi kuliko werevu kwa sababu ya tamaa. Mjinga anaona akitoa 84,000 atapata 200,000 halafu ataingia mitini. kumbe akishatoa 84, 000 hatakaa aone mtu

Hahhahahaha,..

Word mkuu, na ndiyo maana wanalegeza masharti ili uingie kingi!
 
Nilijaribu kufuatilia hili ili kuwajuza Watz akaja mtu mmoja na kumshauri admin aniban na kweli admin akafanya hivyo sijui admin anahusika?basi awaban na hawapia wanaolizungumzia hapa!!
 
Back
Top Bottom