Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,920
Hivi mtu mwenye IQ nzuri na mazalendo mpaka leo hii kweli anahitaji kampeni kujua CCM ndio imetufikisha hapa na tunatakiwa kuikataa?
Unaenda hospitali unakosa dawa alafu bado tu unahitaji kampeni/kuelimishwa kujua kuwa CCM hawafai!!
Mwanao anakosa mkopo na bado huelewi mpaka uelimishwa na wapinzani!
Mazao yako yanaozea shambani bado tu unahitaji kampeni!!!
Unasikia wabunge wa chama tawala wanatuhumiwa kuhongwa milioni 10 na hakuna anaehojiwa alafu bado tu unasubiri kampeni kujia hiki chama hakifai!!
Mwanao,ndugu yako,jamaa yako au jirani yako amekosa ajira baada ya ajira kusitishwa alafu bado tu unasubiri tu wapinzani wa kueleweshe?
Mtumishi hujapata nyongeza ya mshahara,hujalipwa stahiki zako na malimbikizo yako huku makato ya Bodi ya mikopo yameongezeka karibu mara mbii alafu bado tu huewlewi hawa jamaa wanakutia umasikini mpaka wapinzani waje wakueleza haya huku wewe ni msomi na wapinzani wakikaa kimya eti unachagua CCM!!!
Jirani yako asipowapa wanae chakula utamsema vibaya mtaani lakini mkuu wa nchi anapowambia watu wake wanaolalamika kukabiliwa na uhaba wa chakula kuwa serikali yake haina shamba unaona yuko sawa tu mpaka mpinzani aje akuelimisha hii kauli si sahihi na mpinzani akikaa kimya huoni kasoro katika kauli ya mkuu wa nchi!!
.Tangu tupate uhuru huko kijijini kwenu maji ni shida na pengine mna-share maji na wanayama ila kwa miaka zaidi ya hamsini wanakuahidi kukuletea maji alafu hawaleti ila huelewi tu kuwa unadanganywa mpaka mtu mwingine aje apige kampeni na hata akipiga bado tu huelewi!!!
Wabunge wa chama kile kazi yao kubwa ni kusema ndio hata kwa mambo yanayokuumiza wewe mwananchi na wakati wa Bunge live ulikuwa unaoshuhudia kwa macho yako vituko hivi lakini uchaguzi ukija unachagua watu wale wale tena kwa wingi na kabisa unashangilia ushindi wao!!!!
Kwa mifano hiyo michache, haiwezekani IQ yetu ndio ikawa chini kuliko ya watu wa mataifa mengine hapa duniani?
Nadhani kwa sasa tubadili style ya kampeni na badala yake tuje na kampeni za ku-create awareness kwa watanzania wajue wao na nchi yao ni masikini,watumishi waelimishwe kuwa mishaharaa ya ni midogo,nchi yao haina maendeleo ya kutosha,watanzania hawatakiwa kula mlo mmoja kwa siku, hawapaswi kwenda umbali mrefu kutafuta maji, wanao hawapaswi kukaa chini madarasani, hawapaswi kukoso madawa hospitalini,n.k.
Alafu na hawa jamaa wanaojisifia kushinda uchaguzi katika mazingira ya aina hii ya wapiga kura tena pasipo kuwa na tume huru ya uchaguzi huku makada wakiwa ndio wasimamizi wa uchaguzi ni makosa kusema sifa hizi wanazojipa ni sifa za kijinga?
Kuna umuhimu wa kufanya utafiti juu ya IQ zetu na hasa tuki-refer ule utafiti wa mmoja kati ya wanne ni kichaa.