Swali la msingi kwa wapambe wa Magufuli

Swali la msingi kwa wapambe wa Magufuli

Mfukutuzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2015
Posts
239
Reaction score
175
Leo nimekutana na ujumbe wenu mliotusambazia kwenye mitandao ya kijamii, mnatuambia eti Magufuli amepanda ghorofa "saba" kurudisha fomu, sawa sina tatizo hapo

Swali dogo la msingi; "Jengo la NEC lina ghorofa ngapi?"

BAADA YA MAJIBU hapo juu
Ushauri wangu: Angalieni na uongo wa kuwadanganya watanzania, zaidi ya hapo mtazidi kumshusha mgombea wenu badala ya kumpromote

Hata hivyo nadhani hoja ya watanzania si umaarufu wa kupanda ngazi za maghorofa, kwani tumewaambia tunataka wafagiaji wa ofisi, maana hawa ndo hulazimika kupanda ngazi ili wafanye usafi

Mnatutia wasiwasi, yawezekana hata mgombea wenu hajielewi anakurupuka tu, ni kweli tunajua Lowassa kawachanganya ila utulivu ni sehemu ya ushindi, mtapotezana na mtampoteza vibaya mgombea wenu, jifunzeni utulivu mpate kujenga hoja za msingi
 
Mwenyekiti wa ilani ya ccm ni Wasira...
What do you expect?
Kuna wana ccm wenyewe wanataka ife.
 
Labda hawana uhakika na afya yake wakaamua kumpa zoezi.. si unajua alipata kikombe kwa babu? kilichompeleka ni nini?
 
Ndio maana wanatuwekea mitandaoni picha za magufuli akiparamia kwenye miradi ya ujenzi huku amevaa suti!eti iwe ni moja ya sifa utadhani tunatafuta mkandarasi
 
hivi huu nao ni uzi? mods ondoeni hii takataka.

Back
Top Bottom