Swali kwa wanandoa

Nyakwaratony

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2011
Posts
573
Reaction score
140
Hi MMU,

Je kuna tatizo gani iwapo kaka wa bwana harusi mtarajiwa kuwa msimamizi (bestman) wa bwana harusi huyo?

Note: kaka atasimamia harusi hiyo yeye na mkewe.

Ahsanteni.
 
Hi MMU,

Je kuna tatizo gani iwapo kaka wa bwana harusi mtarajiwa kuwa msimamizi (bestman) wa bwana harusi huyo?

Note: kaka atasimamia harusi hiyo yeye na mkewe.

Ahsanteni.
Hakuna baya tena ni bomba sana maana hao watakuwa baba na mama wa ndoa yenu, hakuna tatizo kabisa ............!
 
Inawezekana. Lakini utambue kuwa Wasimamizi wa ndoa yako kwa upande mwingine ni kama wazazi wako kwa ushauri na malezi wakati mnapohitaji. Hivyo watu wengi ikiwepo mimi hupendelea kuwa na wasimamizi wa ndoa ambao sio ndugu.
 
Wala usidhani utakuwa wa kwanza!
 
Ndiyo maana ya kuuliza wanandoa kwani huenda kuna baadhi wamepitia hii situation. Inaweza kuwa na faida ama hasara.
Ndugu yangu embu njoo duniani!
be realistic kidogo!
Ndoa ni yako si ya msimamizi wala wazazi, wala marafiki.
Ni wewe na mkeo. Baaasssss!
Hao wengine wambeya tu,
Utaniita nikusuluhishen, nikitoka hapo kitaaa!
Wasimamizi ni formalities tu za kimapokeo. the way I see it.
 
Wakati wa blues na kulishana keki
wasimamizi pia hubadilishana na maharusi kwa hayo mawili
 
Inategemea na jinsi mnavyojiheshimu kama ndugu wa tumbo moja. Kama mlikuwa hamjiheshimu basi hapo hakuna lolote but kama mlikuwa mnajiheshimu na kaka ana busara za hali ya juu na ni mkubwa kabisa kukiko wewe basi mambo yataenda mswano gwegwe but kama kaka mwenyewe mnazidiana mwaka mmoja au miwili, tegemea kinyume na matarajio yako.
 
Tafuteni couple nyingine yenye kujiheshimu. Nduguyo inakuwa ngumu kumueleza mambo mengine sometimes...
 
Kwangu mimi sioni kama kuna tatizo lolote, kama ni ushauri wa kindoa utatoka kwa viongozi wa kiimani.
 
Wala usidhani utakuwa wa kwanza!
We mkuu GateCrasher endelea tu wala haina shida mkuu. Mie nilifanya hivyo na Sasa maisha yanasonga mbele tu bila shida, kinachotakiwa ni kuhakikisha ya kuwa umechagua mtu kwenye busara na anayejiheshimu. Hata hivyo kama ni matatizo ya kindoa and which are very serious just involve your parents as your final alternative basiii maswala ya kumwambia bestman sijui bestwoman ni mwiko kwa dunia ya Sasa! Jitahidi sana watu wasiijue ndoa yako mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Bibi harusi yupo fine kusimamiwa na shem na mkewe? (hili ni muhimu sana)
kama yupo fine basi hakuna ubaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…