Swali kwa Said Mwema; Alex Masawe na Raymond Shauri uchunguzi wako umeishia wapi?

Nyerererist

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
438
5
Moja ya sifa iliyoingia nayo serikali ya awamu ya nne ni kuupunguza ujambazi ambao ulikithiri na kuhatarisha amani katika baadhi ya miji kama vile Dar es salaam, Arusha na Kilimanjaro. Katika hatua za awali nakumbuka baadhi ya majina ya watu maarufu waliokua wanajihusisha na ujambazi yalipelekwa kwa mkuu wa kaya na kati yao wawili ndio walionekana vinara na tishio katika jamii na hivyo kushikiliwa na kufikishwa mahakamani kwa siku kadhaa.

Naomba niambatanishe Habari ya 09/03/2006 katika gazeti la Nipashe

Alex Masawe, Raymond Shauri ni tishio kwa jamii - Korti

2006-03-09 08:22:16
Na Hellen Mwango na Rosemary Mirondo


Wafanyabiashara maarufu Alex Massawe (50) na Raymond Shauri (45) wako chini ya uangalizi wa mahakama na polisi na kwa masharti magumu.

Walifikishwa mahakamani juzi wakituhumiwa kuwahifadhi majambazi na kupokea mali za wizi wa kutumia silaha.

Hata hivyo hati za malalamiko dhidi yao zimefanyiwa marekebisho na jana zilidai kuwa watu hao ni tishio katika jamii kufuatia kile kilichodai kuwa ni kuwapa fedha na kuwahifadhi majamabazi.

Tuhuma hizo zimo katika malalamiko yaliyowasilishwa na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Polisi katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Uamuzi wa kuwaweka chini ya uangalizi wa polisi wafanyabiashara hao ambao wamekuwa wakishikiliwa na polisi kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja ulifanywa jana na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Umekuja siku moja baada ya mahakama hiyo chini ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi Bw. Francis Mutungi kuahirisha kwa siku moja kesi hiyo ili kutoa muda kwa upande wa mashtaka kurekebisha hati za viapo.

Sehemu ya marekebisho katika hati hizo zinazofanana ilisema ’Alex ni mtu tishio katika jamii, amekuwa na tabia ambayosi njema… anawapa fedha na kuwahifadhi majambazi wanaotumia silaha. Pia anapokea mali zilizoporwa kwa njia ya kutumia silaha.’

Hati hiyo ilisomwa na Mwendesha Mashtaka Inspekta wa Polisi Raphael Rutaihwa ambaye baadaye aliiomba mahakama imweke mlalakiwa chini ya uangalizi wa mahakama na polisi ili asiendelee kuwa tishio katika jamii.

Madai kama hayo pia yalielekezwa kwa mlalamikiwa mwingine (Shauri).

Baada ya maelezo hayo ya upande wa mashtaka, Wakili wao Bw. Peter Swai alisema wateja wake wamekubali kutimiza masharti yatakayotolewa katika dhamana na kwamba wanafanya hivyo kwa kuamini kuwa ni raia wema na hawataki kuisumbua mahakama.

Alidai pia wako tayari kuwa chini ya uangalizi wa mahakama na polisi.

Kufuatia kauli hiyo ya Wakili, Hakimu Bw. Mutungi alisema amegundua kuwa upande wa utetezi hakupinga malalamiko yaliyotolewa na upande wa mashtaka.

’Kwa kuwakumbusha walalamikiwa kuwa tabia zenu za kuhifadhi majambazi na makosa mengi ya unyang’anyi wa kutumia silaha ni hatari…Kama msingekuwa walalamikiwa msingepewa dhamana,’ alisema Bw Mutungi.

Alisema hata hivyo walalamikiwa watakuwa chini ya uangalizi wa mahakama na polisi masharti yanayohusisha kila mmoja kuwa na wadhamini wawili na kwa pamoja naye, watatoa fedha taslimu Sh. milioni 15.

Alisema mmoja wa wadhamini hao anapaswa kuwa na hati miliki ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh. milioni kumi.

Hakimu pia alisema kila mlalamikiwa atasalimisha mahakamani hati yake ya kusafiria na atapaswa asiondoke nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila ruhusa ya mahahakama.

Pia alisema kila mlalamikiwa atalazimika kwenda kuripoti kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Mkoa wa Dar es Salaam kila baada ya miezi miwili.

Kwa mujibu wa Bw Mutungi masharti hayo yatadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia jana.

Hali kadhalika alisema polisi inaweza wakati wowote kuwaita walalamikiwa na kuwahoji.

Baadhi ya wanasheria walizungumzia maana ya hatua hiyo.

’Hii ina maana kuwa sasa watu hawa hawana uhuru, hawana tena usiri. Vyombo vya usalama viko huru zaidi kuwachunguza, vinaweza kwa wakati wowote kuingia kwenye majumba yao na hata magari yao.’ alisema wakili mmoja wa kujitegemea.

Hata hivyo wakili huyo hakutaka jina lake litajwe lakini alisema ni uamuzi wa kawaida wa kisheria na kwamba unafanyika wakati mtu anapoonekana kuwa ni tishio katika jamii.

’Wakibaini kuwa wewe ni tishio, polisi watakukamata hawawezi kusubiri eti litokee ndiyo wakukamate.

Ushahidi wa mazingira unatosha kabisa kuwafanya wakukamate,’ alisema wakili huyo.

Wakili mwingine pia alisema ni utaratibu wa kawaida inapoonekana kuwa mtu fulani ni hatari katika jamii.

’Hatua hii ni ya kumfanya mtu ajilee mwenyewe kwa mambo anayotuhumiwa. Lakini pia Serikali nayo inamlea mtu huyo na kwa wakati wowote ndani ya kipindi kilichowekwa, ikitokea amefanya tukio linalofanana na yale wanayomhisi nayo, lazima akamatwe,’ alisema wakili huyo ambaye naye hakutaka jina lake litajwe.


SOURCE: Nipashe

swali langu kwa serikali na wadau ni kwamba sasa hivi inakaribia miaka miwili tangu hao jamaa wawekwe chini ya ulinzi na wengi wetu hatujui issue yao imeishia wapi na je ilikua halali yao au walionewa kwa manufaa ya kisiasa? jamani sitetei upande wowote lakini nataka "hoja ijibiwe kwa hoja" kama asemavyo mkjj
 
Back
Top Bottom