Kwa kawaida mzigo utatumwa kwenye anuani ya posta utakayoweka (p.o. box) Mara chache baadhi ya wauzaji wanatuma kwa DHL au FEDEX. Ofisi zao zipo ila sina uhakika kama zipo kila mkoa.
Mzigo utakuja kama ulivyouona kwenye picha ila ni muhimu sana usome vizuri maelezo kabla hujaagiza mzigo ili usije ukawa unataka kitu kipya ukanunua used. Vitu kama simu pia lazma usome kama iko locked n.k
Kumbuka mzigo ukifika utatakiwa kuulipia kodi zote stahiki ambazo kwa kawaida hukaribia nusu ya bei ya mzigo.