Mimi ni mzaliwa na mkazi wa Wilaya ya Mbarali. Kuhusu uwepo wa Chadema mbarali ni kwamba ipo lakini nguvu yake sio kubwa na hii inatokana na uzembe wa viongozi,wanaharakati wa chama na wanachama wenyewe kutokuwa commited na kazi ya kukieneza chama maeneo mbalimbali ya wilaya hivyo wananchi kukosa mwamko mkubwa kwa Chadema na ndio maana katika kata ishirini za wilaya Chadema ina kata mbili tu.Lakini nichukue nafasi kuwaomba viongozi na wanachama wa Chadema kuanza kuchangamka na kujitoa kwa moyo ili kuharakisha ukombozi wa Wilaya yetu ili tuweze kukomboka na kupata Elimu,Maji,Afya,Miundombinu mbalimbali,Kilimo bora.Kwasasa nipo nje kwa muda lakini kuanzia mwezi wa saba Nitakuwa Mbarali kuhakikisha harakati zinasonga mbele.Peoples power.