chaUkucha
JF-Expert Member
- May 28, 2012
- 3,382
- 1,212
Siku moja baada ya kuamka asubuhi ghafla kupitia dirishani nilimuona ndege akiwa ametua juu ya tawi la mti. Nikakumbuka ule msemo usemao kwamba ndege wa angani hawana mawazo wala matatizo kama binadamu.
Lakini katika maisha unaweza kumuona mtu usiyemjua akiwa katika shughuli zake akifanya matumizi makubwa au akitembelea magari ya gharama, au mtu mwenye wadhifa mkubwa na jamii inamuita tajiri na yeye akionekana mwenye furaha lakini ukichukua muda wa kuwa rafiki yake na kutembea nae katika maisha yake utagundua kwamba mtu huyo ni kama wengine na ana matatizo na mawazo.
Kisha nikarudi kujiuliza tena swali..... je ni kweli kwamba ndege hawana mawazo/matatizo au ni kwa kuwa hatujatembea nao na kuona wanapopita au shida wanazozipata?