Mlimdharau Mkwawa nilipopata historia yake ya kweli ambayo haijaandikwa
Kumbe alikuwa anatumiwa na waarabu ili kumpinga Mjerumani
Jamaa alikuwa anawakamata watumwa kutoka makabila mengine na kuwauzia waarabu
Alikuwa anapewa zawadi ya kanzu na waarabu anaridhika
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza nadhani waliofanikiwa kukipata kichwa chake walitaka kwenda kuwathibitishia wakubwa wao kuwa huyu ndiye mtu aliyetusumbua Sana na kuuwa watu wetu wengi,na huenda walipandishwa vyeo kwa ushujaa huo,lakini Jambo la pili ni kulitunza fuvu kama ishara ya kuwakumbuka wenzao waliouwawa kwenye vita vile pamoja na kuiondoa kumbukumbu kwa watu wa jamii ya Mkwawa na vizazi vyao. Haya ni maoni yangu.
Kuna society inaitwa,SKULL&BONES..
Hawa hufanya matambiko ya kunywa damu ,Kama sikosei za watu,Hilo fuvu hutumika Kama kikombe.
Wakishafanya matambiko hayo wanna maintain power.
Kwahiyo ruling elite wengi mfano Rais Bush ni member wa skull&bone society
History..!! Nonsense subject.Mtemi Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga ni moja kati ya wahenga wetu wenye historia kubwa sana ya ushujaa hapa Tanganyika, nadhani kwenye orodha yangu namuweka na wakina Mirambo pamoja na Abushiri.
Mtemi Mkwawa alipigana vita kubwa na makabila yaliyoogopeka hapa Tanganyika, kuna kipindi Chabruma chifu wa Wangoni kabila ambalo liliogopeka kusini yote alijaribu kumchokonoa alitafutwa sana hadi akaenda kujificha.
Pia inasemekana Wamassai ambao walipiga makabila mengi ya Kaskazini walipojaribu kushuka Kusini walikutana na vikosi vya Mkwawa mpakani mwa Himaya yake kule Morogoro. Wamassai na ubabe wao wote walitulizwa hadi wakakubaliana na Mkwawa kwamba hawatashuka Kusini.
Nakumbuka niliwahi kusoma nyaraka fulani miaka ya nyuma kidogo ambapo wanajeshi wa Ujerumani walisema hivi kuhusu wahehe "these people know nothing than war, it's like they bred only to fight wars".
Wakati anapigana na Wajerumani kilichowashangaza zaidi ni pale ambapo alitumia mkakati (Strategy) ambao ulitumiwa na Napoleon Bonaparte kwenye Vita ya Mapiramidi kule Misri. Ule mkakati ndiyo unamfanya Napoleon aitwe Military Genius mpaka leo.
Swali nalojiuliza ni hili: Nini kiliwafanya Wajerumani wachukue fuvu la Mtemi Mkwavinyika na kulipeleka kwao Ujerumani? Sababu kubwa hasa ni nini?
Nakumbuka huu mchezo ulifanywa hadi kwa chifu wa Wahindi wekundu Geranimo ambaye alipambana sana na wazungu kulinda ardhi yao isinyanganywe. Walikata fuvu lake na kuondoka nalo kusikojulikana.
Ok,cheki encyclopedia
View attachment 1299568
Yes, to people who are living dead.History..!! Nonsense subject.
.
Sisi tupo hapa tunawasoma wakuu.
Alikuwa anapewa zawadi ya kanzu na waarabu anaridhikaMlimdharau Mkwawa nilipopata historia yake ya kweli ambayo haijaandikwa
Kumbe alikuwa anatumiwa na waarabu ili kumpinga Mjerumani
Jamaa alikuwa anawakamata watumwa kutoka makabila mengine na kuwauzia waarabu
Alikuwa anapewa zawadi ya kanzu na waarabu anaridhika
Sent using Jamii Forums mobile app