Swali anaweza pata nafasi ya kusoma diploma na cheti cha form 4 kwa vyuo vya ufundi kama DIT, MUST..

Kijana Jr

JF-Expert Member
May 12, 2016
560
843
Wakuu heshima kwenu,
Kuna kijana hapa mtaani ameniomba ushauri nimeleta kwenu maana dah story yake ni ndefu na yakuhuzunisha in short.

Ni kijana wa miaka 23 alimaliza form four mwaka 2011 na matokeo yake alipata Four ya 33, D mbili(History D,& Geo D). Wakati akiwa form 3 alipatwa na ugonjwa wa kutosikia (uziwi) ambao ulichangia kumnyima ability ya kujiamini.

Baada ya kumaliza shule akaanza taratibu za matibabu, akaenda Amana na hospitali kibao mpaka nyumba za ibada akahangaika. Ndani ya miaka miwili Mungu akamjalia tatizo lake likapungua kidogo ila hakupona kabisa.

Kijana alitamani arudi shuleni ila kutokana na uwezo wa familia yake ni mdogo ikashindikana akaona ni bora akajiendeleze kusoma kuliko kukaa nyumbani basi akajiunga na chuo cha ufundi VETA fani ya umeme mwaka 2014 ,akamaliza mwaka jana 2015 kwa kufanya mtihani wa level 2 na kufaulu masomo yake vizuri katika mfumo wa C B A.

Wakati akiwa College VETA alijenga urafiki na mwalimu mmoja ambaye alivutiwa na uwezo wake wa kuelewa japo hasikii vizuri. Kuna siku yule ticha akamsihi kwanini asirudi sekondary akaanze form two. Kijana akamueleza sio kama sipendi kusoma tatizo nyumbani uwezo hakuna. Yule ticha akamwambia kijana utasoma ila huko mbeleni utapata shida kwenye masomo kwa maana kuna vitu vitakukatisha tamaa, inabidi urudi sekondary ukaanze form 2 ukasome sayansi vizuri mpaka form 4. Kutokana na kukuamini utapita na kufika form six mpaka chuo nakutimiza ndoto yako ya uhandisi wa umeme nenda katafuta shule kisha uniambie kuhusu malipo mimi nitashughulikia kutafuta mdhamini wa kukusomesha.

Kwa upande wa kijana anapenda kuwa mtaalamu wa Electrical &Electronics kama utapata bahati ya kusoma mpaka diploma &degree.

Pia kama haitambana sana anapenda kuja kuwa teacher wa masomo ya sayansi primary, sekondari,au college aje kusaidia people who have special needs (walemavu wa viungo), kutokana na yeye kulionja kojo la ubaguzi
na changamoto.

Sasa swali ni hivi anaweza pata nafasi ya kusoma diploma kama akipata level 3 na cheti chake cha form 4 kwa vyuo vya ufundi kama DIT, MUST, Arusha Tech.
Je na huyu ticha akipata mdhamini, aende sekondary? Kwani ukicheki umri nao unakwenda.
asanteni
 
Mwambie apige level 3 akimaliza aende MUST akasome diploma ingawa atapitia kozi fupi ya miezi kama 4 au 3 yakumuandaa kusoma diploma level 4-6 miaka 3.
 
Back
Top Bottom