Ndondwa
Member
- Jan 7, 2016
- 46
- 12
NAWAZA! NAWAZA SANA HATIMA YA VIJANA WA TANZANIA.
Sikumbuki vizuri, lakini kabla ya miaka ya 2000's ilikuwa kawaida kuona kata nzima ikitoa wanafunzi 1-3 kuendelea na masomo ya sekondari mara baada ya kuhitimu elimu ya msingi (ref kata yangu ya Matema (W) Kyela)
Sababu kubwa ya idadi ndogo sana kuendelea na masomo ya sekondari ilikuwa ni uhaba wa shule za sekondari nchini, ambapo, kabala ya miaka ya 2000's (W) ya Kyela ilikuwa na shule za sekondari mbili, Itope na Kyela day.
Nashukuru serikali kwa sera ya elimu ya 1995 ambayo ililenga kuongeza shule za sekondari angalau kwa kila kata, Jambo ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana , ambapo kwa sasa tuna shule za serikali takribani 14 na shule za watu binafsi kama 3 hivi ka sijakosea.
Kujengwa kwa shule hizo kumesaidia kuongezeka kwa wanafunzi wanajiunga na masomo ya sekondari kiasi kikubwa sana na kufanya elimu kuwa haki ya kila mmoja (mwenye sifa).
Miaka ya hivi karibuni jamii imeshuhudia ongezeko kubwa sana la idadi ya watu kutokana na kuzaliana kwa kasi sana. Ongezeko hilo limefanya VIJANA kuwa wengi zaidi mtaani kuliko kawaida.
Hao ni VIJANA walio wengi ambao wameenda shule (msingi/sekondari) lakini wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na kukosa sifa za kuendelea na masomo ya ngazi inayofuata na kuwaacha bila maarifa yoyote ya kuwawezesha kuyamudu maisha mtaani.
Ndani ya idadi hiyo ya vijana, wapo ambao wanajiona ni wasomi kuliko wengine (form IV V/s STD 7). VIJANA hao wanajiona wasomi wanaungana na kundi lingine kubwa la wale waliokuwa na sifa ya kuendelea na masomo mpaka kufikia elimu ya vyuo katika ngazi mbalimbali..
Kutokana na kuwepo kwa fursa chache za kiuchumi au miundombinu ya kuwafanya VIJANA wakajiajiri wenyewe katika mazingira yao kumesababisha mlundikano mkubwa wa VIJANA wasio na ajira.
Serikali imekuwa ikijaribu sana kufungua milango ya fursa ambazo zingezalisha ajira kwa VIJANA bila mafanikio yoyote. Mimi nadhani sera za ajira kwa VIJANA zimeshindwa kufanya kazi kutokana na sababu kubwa mbili, ya kwanza ni kutokuwepo kwa mapinduzi ya kilimo na baadae viwanda, na kukosa viongozi wa kutekeleza sera hizo.
Kwa sasa serikali inakuja na matamko ya kuwafanya VIJANA wafanye kazi lakini bila kuwaandalia mazingira ya kufanyia hizo kazi.
Mwaka 2015 wakati wa kampeni nlikuwa nasikiliza kwa makini sana sera za wagombea haswa wa CCM na CHADEMA. Sera zilikuwa nyingi lakini nilivutiwa sana na sera ya ajira kwa VIJANA, ambapo JPM kwa upande wake alijinadi kufufua viwanda vilivyo kufa na kujenga vingine vingi ambavyo alisema VIJANA watafanya kazi humo.
Ahadi hiyo ni nzuri lakini nashindwa kuelewa kwamba itatekelezwa vipi akati hakuna sera nzuri ya kufanya mapinduzi ya kilimo (hakuna mapinduzi ya viwanda bila ya mapinduzi ya kilimo kuanza). Rejea Agrarian Revelution na baadae Industrial Revelution.
Kwa upande wa CHADEMA nilisikiliza pia, huku EL naye akijinadi kutegua bomu hili la ajira kwa vijana, alizungumza mengi sana ambayo mengi sana yanafanana na yale JPM.
Kitu cha pekee nilichovutia sana ni kile EL ambacho alisema kuifanya JKT kuwa sehemu yakuzarisha VIJANA wenye ujuzi mbalimbali na si tu mazoezi ya ukakamavu. Katika maelezo yake alidadavua kuwa angepeleka vifaa vya mafunzo ya VETA JKT ili VIJANA wajifunze mafunzo mbali mbali ya ufundi na kufungua mabalaza ya Sanaa na michezo kila wilaya ambalo lingeshughulika nakutafuta VIJANA wenye vipaji na kuwawezesha kujiajiri wenyewe watakapo rudi mtaani.
Kwa maelezo mafupi hapo juu,mimi naona ni muda mwafaka wa serikali ya Tz kuitumia JKT kama kiwanda cha kutengeneza VIJANA wenye ujuzi mbalimbali ili baadae wasaidie kusukuma kurudumu la maendeleo kwa kasi.
Serikali inatakiwa kuwatambua VIJANA wote mahali walipo na kuendesha aundikishaji maalumu wa VIJANA watakao jiunga na JKT ili kwenda kujifnza stadi mbali mbali (hawa ni muhim wawe wale walishindwa kuendelea na masomo) na iwe lazima kwenda huko.
Faida ya programu hii utakuwa kubwa badae maana taifa litajawa na VIJANA wengi wenye ujuzi, nidhamu na Uzalendo kwa taifa lao na kikubwa zaidi nchi haitapata shida ya kupata walinzi wa taifa (wanajeshi) kwani watapatikana miongoni mwao na tatu, tatizo la ajira litakuwa limepungua kwa kiasi kikubwa sana.
Naiomba Serikali iangalie namna nzuri ya kusaidia VIJANA kuliko kutoa mashinikizo ambyo baadae kwa namna moja au nyingine itageuza hata VIJANA wema kuw waharifu. Hii ni kwa sababu, ukisema kijana aache kucheza pool table asubuhi badala yake wakafanye kazi, tujiulize, wakafanye kazi wapi? Je kuna miundombinu ya kusaidia wao kufanya kazi?
Hitimisho, Tanzania bado ni nchi changa sana lakini yenye rasilimali nyingi za kufanya iendelee bila kutupia macho mataifa ya nje kuomba misaada. Yafaa kuwekeza kwa VIJANA wetu ambao wao angalau maisha yao bado marefu, hii itasaidia kuwa na SUSTAINABLE DEVELOPMENT ambapo wataalamu wanabainisha kuwa SUSTAINABLE DEVELOPMENT is that, the FUTURE should be BETTER than TODAY.
Kama kuna mapungufu ya hoja yangu ni ruhusa kuongeza kilicho pungua au kutoa pendekezo zuri zaidi ili kusaidia taifa letu. NAKUPENDA TANZANIA
Ahsante