Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
"Nitawashughulikia hata maaskari wanaobambikia watu kesi hovyo hovyo hakika sitawaangusha. Kama niliweza kusimamia sheria nikiwa waziri tu, sasa niwe rais kabisa...hiiiiiiiiii...(vicheko vya wananchi wa Mara vilisikika)."
Hiyo ilikuwa ni kauli ya Mhe.
Magufuli alipokuwa katika moja ya mikutano yake mkoani Mara. Sasa juzi juzi hapo kumekuwa na tukio la kutunguliwa kwa ndege ya doria huko Maswa jambo lililozua utata mkubwa sana na huzuni kuu kwa Watanzania na Waingereza kwa kuwa rubani huyo alikuwa raia wa Uingereza.
Kuanzia siku ya juzi kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusiana na kukamatwa kwa walioitwa watuhumiwa wa ujangili na utunguaji wa ndege hiyo. Nimejaribu kuperuzi na kufanya mawasiliano ya kina kutoka kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya hifadhi na nimepata taarifa kuwa kulikuwa na upekuzi wa nyumba baada ya nyumba ikiwemo vitisho vya hapa na pale kwa wananchi kusudi wawataje watu wanaowahisi kuwa majangili au wamiliki wa silaha kinyume cha sheria.
Hofu yangu kuhusiana na waliokamatwa ni kwamba, isijekuwa ni FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE ya jeshi la polisi kwa lengo la kutaka waonekane wanafanya kazi kwa kukamata kamata hata wanyonge wasiokuwa na hatia. Ukitazama vema sura za waliokamatwa hazifanani kabisa na uwezo, maarifa na ujuzi wa kutungua ndege japokuwa yawezekana mmoja au watatu kati yao walishiriki.
Ikiwa wana makosa mengineyo sawa lakini si vema kumhusisha kila raia anayekaa na hifadhi na suala la utunguaji wa ndege.Natoa rai kwa jeshi la polisi kuchunguza kwa umakini jambo hili na kuhakikisha wanakamatwa majangili wa kweli na siyo wanyonge wanaowinda nguruwe pori kwa ajili ya kitoweo.