Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,998
- 20,358
Nimesikiliza HUTUBARI nyingi, 11/01/2017 nimemsikiliza kijana wa Kijaluo mwenye makazi ya kudumu jijini Illinois huko unyamwezini, amesisitiza Wamarekani kuizingatia vizuri siasa kwakuwa ulimwengu na maisha yao vimo ndani ya siasa, ajabu kwenye ka-inji kakufikirika mtawala wake anasema siasa yeye hataki kabisa, yaani anataka kuwa kama ngariba wa kijijini kwetu Nyang'oro Tarime anayeogopwa nakusikilizwa kwakila awazalo na kuota. pia leo huko kwenye ka INJI kakusadikika wao wanasema kainji ka vi-wonder, kwakweli nimebaki kucheka tu huku machozi yakinibubujika, si kwafuraha bali furaha yabisi...
Nimekumbuka mbali sana, imenilazimu kurejea historia ya nchi za kale zilizopita katika tawala za aina hiyo, nimemkumbuka Sheikh Abeid Karume aliyetawala nchi bila katiba tangu alipopewa nchi na Julius Nyerere pale Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam Tanzania, utawala wake ulikuwa unafanana sana na kainji haka ka leo, utawala ulikuwa wa kauli tu,
Tangu Mapinduzi ya Januari 12, 1964, Zanzibar haikuwa na Katiba wala Sheria; iliongozwa kwa Amri za Rais- (Presidential Decrees) kadri alivyoona inafaa.- Na kwa mujibu wa Gazeti la The Tanganyika Standard la March 9, 1968, Karume aliapa kutofanya uchaguzi wala kuwa na Katiba Kisiwani kwa miaka 50 tangu 1964 - 2014 Kwa madai kwambachaguzi zote ni vyombo vya mabeberu kuwakandamiza wananchi.Na kadiri kalamu ya Karume ya wino wa damu ilipozidi kuandika historia ya ukatili, udikteta na umwagaji damu kwenye kurasa ngumu za kukwaruza ndivyo alivyojichongea na kujiongezea upinzani na uadui kwa jamii ya Kizanzibari.
Kulikuwana vuguvugu ama tuseme harakati za hapa na paleza kupinga utawala wa Karume ambazo Utawala wa Karume ulitumia mwanya huo kuziita ni majaribio ya hapa na pale ya kutaka kuiangusha Serikali ya Karume kuanzia mwaka 1964.Thabit Kombo Jecha katika “Simulizi”anayataja baadhi, likiwamo lile la Desemba 1964 lililoongozwa na Amour Zahorwa Unguja, la 1967 likiongozwa na Suleiman Hamad Suleimanwa Pemba, la 1967 tena, likiongozwa na Saleh Ali Nassorwa Unguja, na la 1968 likiongozwa na Salim Mohamed Abdullah wa Pemba.
Kufikia mwaka 1967 hofu ya Karume dhidi ya wenzake na kwa nafasi yake ilitia fora kiasi cha kuogopa kivuli chake mwenyewe. Na ili kuendelea kuwamaliza wenzake, mwaka huo zilitungwa tuhuma za uongo dhidi ya watu 14 makada wa ASP katika kumpindua, zikiwalenga hasa wenye fikra za kikomunisti.
Walioingizwa kwenye tuhuma hizo ni pamoja na mawaziri wa Serikali yake mabwana Abdallah Kassim Hanga, Salehe Saadallah Akida, Abdul Aziz Twala na makatibu wakuu wa wizara, Aboud Nadhif na Mdungi Ussi na baadaye Othman Sharrif.Wote waliokuwa Visiwani walikamatwa, kisha wale walokuwa bara, Karume akamuomba Nyerere kuwarejesha Zanzibar kutoka Bara ndugu Othman Sharrif na Kassim Hanga ili "wakahojiwe" lakini wote wakaishia kuuawa kikatili baharini bila kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mmoja wa mashahidi wa uongo walioandaliwa dhidi ya watuhumiwa kwa vyombo vya Karume, alikuwa Ahmada ambaye kwa uongo wake, watu wanne akiwamo Hanga, Twala, Saadallah na Othman, walinyongwa mwaka 1969.- Kwa uongo huo, Ahmada alizawadiwa cheo cha kapteni jeshini.- Ni Kapteni Ahmada huyu, aliyeshiriki kwenye mauaji ya Karume miaka mitatu baadaye.
Kwa hofu ya jamii ya Kizanzibari kufikiwa na fikra na mawazo mapya ya kimaendeleo, Karume alipiga marufuku vijana wa Kizanzibari kwenda nje kwa masomo ya juu ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam; alipiga marufuku pia ujenzi wa Chuo Kikuu Visiwani. Karume alitumia kikosi madhubuti cha Usalama wa Taifa Zanzibar maarufu kama viwavijeshi ambao walimtii hata akipiga chafya tu.
Mbali na kutokuwapo kwa utawala wa sheria enzi za Karume, unyanyasaji wa kijinsia na ubaguzi kwa misingi ya historia na kisiasa ulitia fora. Kwa mfano, mwaka 1966, alitoa amri (decree) kuwanyima wazazi haki ya kuwakataa wanaume walioposa binti zao kama njia ya kuondoa ubaguzi wa rangi. Kwa sababu hii, wasichana, hasa wale wa Kiarabu walilazimishwa kwa nguvu ya Serikali kuolewa kwa nguvu. Karume mwenyewe, wakati huo akiwa na umri wa miaka 65, aliwania kuoa kwa nguvu, wasichana wanne wa Kiajemi, na alipokataliwa, aliamrisha wazazi wao watiwe kizuizini na kuchapwa viboko kwa kosa la kuzuia mpango wa ndoa mchanganyiko, na baadaye kutimuliwa Zanzibar.
Chini ya mpango huo, raia wa kigeni waliotaka kuchumbia wasichana wa Kizanzibari walitakiwa kuilipa Serikali Sh. 64,000,000, bila hivyo hawakuruhusiwa kuwaoa. Karume alikuwa ameanza kuwa mwiba kwa Mwalimu Nyerere pia juu ya Muungano. Kwa mfano, alimkatalia Nyerere kwa lugha ya dharau na kejeli juu ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na Azimio la Arusha kutumika Zanzibar.Na kuhusu akiba ya fedha za kigeni ya Zanzibar iliyofikia dola milioni 80 mwaka 1972, alimuonya asithubutu kuitolea macho, akamwambia:- “Fedha ya kichwa cha Malkia si yako na usiniulize, labda niulize juu ya hii (sh.) yenye picha ya kichwa chako.
Na kuhusu Muungano, Karume alikuwa ameanza kuchoka nao. Siku moja alisema, Muungano ni kama koti tu; likikubana unalivua. Ufa huu kati ya viongozi hao wawili juu ya Muungano, ndio uliosababisha kamati ya kupendekeza Katiba (Constitutional Committee) isiundwe na Bunge la Katiba (Constitutional assembly) lisiteuliwe ndani ya muda wa mwaka mmoja tangu Muungano, kama ilivyotakiwa chini ya Mkataba wa Muungano wa Sheria ya Muungano ya 1964. Wadadisi wa mambo ya siasa wanakubaliana kuwa, kama Karume angeendelea kutawala miaka kadhaa baada ya 1972, Muungano ungefikia kikomo kwa njia ya kutisha na kusikitisha.
Kufikia mwaka 1972, upinzani kwa Serikali ya Karume ulikuwa umechukua harakati za uasi wa umma, chini kwa chini kwa mara ya kwanza tangu Hanga na wenzake wanyongwe mwaka 1969.Kwa vigezo vyovyote vile vya utawala na uongozi, Karume alitawala kwa mkono wa chuma; alitawala kidikteta katika nyanja zote za maisha ya Wazanzibari kisiasa, kiuchumi na kijamii.-- Alikuwa kero pia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kwa Muungano. Karume aliuawa kikatili kwakumiminiwa risasi kifuani.
Ukiacha Karume, nimemkumbuka Haile Selasie kiongozi wa zamani ya Ethiopia, huyu alitawala nchi kama yupo ndani ya box, alikuwa haambiliki wala hasikii la mnadi swala wala mpiga azana, taifa lilipokumbwa na njaa aliinuka kwa kejeri na kusema taifa lake halina njaa wanaosema kuna njaa ni waongo na wafitini tu, na zaidi akatoa marifuku ya tangazo lolote la njaa kupitia tangazo la serikali maarufu namba 12349. Watu wakafa njaa, mifugo ikafa, ukame ukalikumba taifa na hatimae akauwa yeye kwa aibu kubwa...
Sikuishia hapo nimemkumbuka Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga, huyu alijiita Mungu wa Wakongo, aliamini dunia ni yake, aliamini maisha aishiyo yeye ndio waishiyo Wakongomani, alivuka mipaka akatoa amri kuwa migodi ya Katanga yote itakuwa yake asiguse mtu, na migodi ya kwingineko huko kila mwenye nguvu akachimbe awezavyo, huku taifa likikumbwa na njaa, aliamua kununua pambano la ndondii la bingwa wa dunia Mohamad Alli lililokuwalifanyike Dallas Nchini Marekani akalihamishia Kinshasa Afrika, hakuishia hapo, bali huku taifa likiwa na dhiki kubwa, yeye alinunua ndege kubwa kuliko zote duniani aina ya congodi mpya toka kiwandani nchini Ufaransa, hii aliifanyia kwa starehe zake na familia yake na wapambe. Mobutu alikufa kifo cha aibu....
Leo naiona sura kali ya watawala wale katika nchi ile ya kusadikika, nchi ile iliyopembeni mwa Bara la Kuwait, Watala wote hapo juu ilikuwa ni marufuku kuwakosoa, ilikuwa ni kosa kubwa kama vile uhaini, na adhabu kubwa ilikuwa ni kifo. Waliendesha mauaji ya kimyakimya kwa wapinzani, mshakama zilijaa kesi za kisiasa, kibaya zaidi mahakama zote zilikuwa chini ya amri za watawala hao wakale, yanj wao walikuwa ni miungu watu katika nchi zao.
Naona watu wamepata rais au watu wamepatikana, huenda ni njia anayoamua Mungu wa watu wale na taifa lile kuwapitisha kwenda kwenye nchi ya vi wonder walivyoahidiwa. Kimsingi kanuni ya kujenga balipojengwa inasema huwezi kujenga bila kubomboa kwanza, naam..... taifa linabomolewa ili lijengwe taifa jipya na watu wake wapya....Atakayekuja kulijenga taifa sio huyu anayelibomoa, yupo mtu kati ya watu wale aliyechaguliwa na Mungu wao kuja kulijenga taifa lake.
Pole ndugu zangu Wanyarwanda na Warundi.