Supp sio kilema, tunasapua tunasepa

mtanganyika wa kweli

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
2,420
1,718
*SUP SIO KILEMA*


Sup kwangu si kilema,
Ni matokeo ya kitaaluma,
Kama kusoma nilisoma,
Mtihani nikajibu vema,
Moduli zote zilituama,
Imenitokea haijaniuma,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

Sup ipo *UDOM*,
Mzumbe hadi *SAUT*,
Sup ipo *UDSM*,
Makumira hadi *NIT*,
Sup ipo na *MUM*,
Hadi Mtwara ya *SAUT*,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

Sup ipo kwa *walimu*,
Madaktari na *mafamasia*,
Sup ipo kwa *mahakimu*,
Hadi wale *mainjiania*,
Wahasibu na *Masikomu*,
Wanasiasa na *wanasheria*,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

Yawahenga nayakumbuka,
Leo kwangu kesho kwako,
Wewe unayenicheka,
Kesho ni zamu yako,
Usijione umekamilika,
*UE sio mjomba wako*,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

Tuunde na makundi,
Kwa pamoja tujadili,
Hata sisi hatupendi,
Imetokea kama ajali,
Tulihudhuria vipindi,
Biology na Kiswahili,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

Wapo waajiriwa,
Walisup wakasapua,
Wapo wahemishiwa,
Walisup wakasapua,
Wanasup sije pagawa,
Semista ijayo tutatoboa,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

Wala usije jificha,
Ukasingizia eti spesho,
Huo uoga jaribu acha,
Ili usisup tena kesho,
Iwe semina iwe lekcha,
Jitahidi kuvuja jasho,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

*Si kilaza si kipanga*,
Yote amepanga Mungu ,
Tena Sup Sio ujinga,
Nisikilizie Rafiki yangu,
Tena Sup wala si janga,
Nitapata degree yangu,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*


 
Kwetu ilikuwa inaitwa Summer Conference......Kupunguza ukali wa maneno.Mapema watu wameshajuana wazee wa Summer Conference (utasikia safari hii ninazo chache 3 tuu,mwingine daah mie zipo 2 na kipolo kimoja).Uzuri Sup.inakufanya uwe NONDOOOO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom