Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,406
SUNGURA KACHOMOKA.
1)Wameona walobisha,taratibu wanakaa.
Nafasi waliipisha,walipowasha mkaa.
Tufe wakabiringisha,kwa uzuri wa chokaa.
Sungura amechomoka,nyumbu wanatapatapa.
2)kiti moto chaunguza,kigumu kukikalia.
Bucha alishaiuza,kimya kimya mwajilia.
Chozi analipuuza,washamba wafutahia.
Sungura amechomoka nyumbu wanatapatapa
3)naona kifo cha panya,mende cha mkaribia.
Nzi wanajidanganya,mzinga kaujengea.
Ya kale kwa mandonya,poa kama mwachafua.
Sungura amechomoka,nyumbu wanatapatapa.
4)pole kwa huo msiba,kaburi mwalifukua.
Ila kidogo si haba,jama alipendezea.
Ameshachoro mraba,mwaanza kuozea.
Sungura amechomoka,nyumbu wanatapatapa.
5)fata mkumbo kitumbo,kitambi chanza pungua.
Umeshapikwa urimbo,ndege mmeunasia.
Poleni japo ni pambo,kwa ndani mnaumia.
Sungura amechomoka,nyumbu wanatapatapa.
Shairi=SUNGURA AMECHOMOKA.
Mtunzi=Idd Ninga wa tengeru arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
1)Wameona walobisha,taratibu wanakaa.
Nafasi waliipisha,walipowasha mkaa.
Tufe wakabiringisha,kwa uzuri wa chokaa.
Sungura amechomoka,nyumbu wanatapatapa.
2)kiti moto chaunguza,kigumu kukikalia.
Bucha alishaiuza,kimya kimya mwajilia.
Chozi analipuuza,washamba wafutahia.
Sungura amechomoka nyumbu wanatapatapa
3)naona kifo cha panya,mende cha mkaribia.
Nzi wanajidanganya,mzinga kaujengea.
Ya kale kwa mandonya,poa kama mwachafua.
Sungura amechomoka,nyumbu wanatapatapa.
4)pole kwa huo msiba,kaburi mwalifukua.
Ila kidogo si haba,jama alipendezea.
Ameshachoro mraba,mwaanza kuozea.
Sungura amechomoka,nyumbu wanatapatapa.
5)fata mkumbo kitumbo,kitambi chanza pungua.
Umeshapikwa urimbo,ndege mmeunasia.
Poleni japo ni pambo,kwa ndani mnaumia.
Sungura amechomoka,nyumbu wanatapatapa.
Shairi=SUNGURA AMECHOMOKA.
Mtunzi=Idd Ninga wa tengeru arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com