figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Analalamika kadozi kenyewe kadogo tu. Hivi anajua maumivu waliyopitia wapinzani enzi yuko upande wa watesi?Sumaye huyu, "... ukitaka mambo yako yafanikiwe njoo CCM" - Naikumbuka kauli hii ya kifedhuri. Acha aumizwe, wametuumiza sana wakiwa upande ule.... simuonei huruma japo yuko upande wetu sasa. What goes around... hata watesi wetu wa sasa kuna muda watakuwa kama Sumaye... Historia ni mwalimu mzuri sana.
Kuna utaratibu unatakiwa kufuatwanchi nzima ilani inayotekerezwa ni ya ccm, na ndio waliounda serikali, hata huyo meya anatekereza ilani ya ccm kupitia halmashauri aliyopo. wakwenda kukagua utekerezaji ni ccm na si vinginevyo. huo ndo ukweli.
Tatizo la hawa wanaona kama ndio wamiliki wa hii hii nchiKwa hiyo polepole anapozunguka hakuna kosa jinga sana wewe
Swissme
Chadema haipo juu ya sheria na utaratibu
Hawezi kuingia bila taarifa kwenye ukumbi wa halmashauri wakiwa na sare za chama kisha kufanya vikao!
Walipaswa kufuata utaratibu
Pia Sumaye hana wakumtisha
Aache kutoa hizo kauli za kijinga
Kwenda kukagawa madiwani wanavyotekeleza ilani ya CCM ni kosa?.nchi nzima ilani inayotekerezwa ni ya ccm, na ndio waliounda serikali, hata huyo meya anatekereza ilani ya ccm kupitia halmashauri aliyopo. wakwenda kukagua utekerezaji ni ccm na si vinginevyo. huo ndo ukweli.
Sumaye ameiomba Serikali iache kuwafanyia fujo CHADEMA. wanayo haki ya kutembelea Sehemu walizoshinda ili kuona kama kweli Madiwani wao wanafanya kazi walizowaahidi wananchi.
Pole Pole ni Chama chenye dola ...1Kwa hiyo polepole anapozunguka hakuna kosa jinga sana wewe
Swissme
Miaka yote hakukuwa na Ilani .................!!?nchi nzima ilani inayotekerezwa ni ya ccm, na ndio waliounda serikali, hata huyo meya anatekereza ilani ya ccm kupitia halmashauri aliyopo. wakwenda kukagua utekerezaji ni ccm na si vinginevyo. huo ndo ukweli.
Upumbavu ni kufanya mambo bila kuzingatia sheria ukategemea utaachwa eti kisa una kitambi!Hata kama mie sio mwanasiasa, nakubaliana na Sumaye kwamba serikali sasa imeanza kufanya mambo kwa ujinga na upumbavu. Hii kamata kamata ya viongozi wa upinzani inapita mipaka sasa. Nimeona wakimzuia Meya hapa Dar, na polisi kumsubiri mlangoni mwingine kule Arusha kwa masaa zaidi ya sita wamkamate baada ya kikao.
Huu ni uumbavu na ujinga unaofanywa, naamini, kwa shinikizo la viongozi wa CCM, ambao hautaleta hali nzuri kwa nchi yetu - ukosefu wa amani kwa sababu tu tuna siasa za vyama vingi. Na bado tunashuhudia ujinga mwingine ukiendelea Bungeni.
Kama Magufuli anaona siasa za vyama vingi nchini hazifai, basi tufanye referandum tena kuamua kama turudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Lakini ujinga na upumbavu wa namna hii hauna manufaa hapa nchini.
Hakuna demokrasia ya kujidai wewe ni mkagua miradi ambayo hujaitolea hela na wala hukuipanga.Kama hawataki basi wafute vyama vya upinzani kila maali kamatakamata inakera Sana sasa hii ndio demokrasi gani eti nchi ya amani
Kawachoma msumari WA mottoHeshima kwenu wakuu,
Sumaye ameiomba Serikali iache kuwafanyia fujo CHADEMA. wanayo haki ya kutembelea Sehemu walizoshinda ili kuona kama kweli Madiwani wao wanafanya kazi walizowaahidi wananchi.
Hapa Ubungo kuna diwani wa CHADEMA, sisi kama Viongozi wake tumekuja kuona utendaji wake je anafanya kazi kweli au hafanyi. Sasa kosa lipo wapi?
Polepole na Bulembo wa CCM wanazunguka kila Halmashauri nchi wala hawakatazwi na haiwi nongwa. Lakini chadema wakitembelea pale wanapoongozwa wanakamatwa wanatiwa ndani.
Tunaomba Serikali ituache tuwatumikie wale waliotuchagua sababu hii miradi tunayoitembelea sio ya Chadema tu bali itatumiwa na Vyama vyote.
"Tunaomba tu Serikali ituvumilie, CHADEMA ni chama halali kisheria na kinafanya kazi yake yake kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi" Mjumbe Kamati Kuu CHADEMA na Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Frederick Sumaye.
MY TAKE:
Mjusi ukimkimbiza sana akifika ukingoni ambapo mbele hakuna njia tena, hugeuka nyoka na kuanza kukukimbiza wewe. Siasa CCM wanazofanya hazijawahi kufanikiwa sehemu yoyote Duniani. Kwamba mshindani wako unamfunga mikono kwa nyuma halafu unataka mpande ulingoni kupambana kisha unajisifu umeshinda. Ni kutojitambua na ni aibu.