Sumaye: Serikali itambue CHADEMA ipo kisheria, wasitake vurugu bila sababu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
19,540
23,936
Heshima kwenu wakuu,

Sumaye ameiomba Serikali iache kuwafanyia fujo CHADEMA. wanayo haki ya kutembelea Sehemu walizoshinda ili kuona kama kweli Madiwani wao wanafanya kazi walizowaahidi wananchi.

Hapa Ubungo kuna diwani wa CHADEMA, sisi kama Viongozi wake tumekuja kuona utendaji wake je anafanya kazi kweli au hafanyi. Sasa kosa lipo wapi?

Polepole na Bulembo wa CCM wanazunguka kila Halmashauri nchi wala hawakatazwi na haiwi nongwa. Lakini chadema wakitembelea pale wanapoongozwa wanakamatwa wanatiwa ndani.

Tunaomba Serikali ituache tuwatumikie wale waliotuchagua sababu hii miradi tunayoitembelea sio ya Chadema tu bali itatumiwa na Vyama vyote.

"Tunaomba tu Serikali ituvumilie, CHADEMA ni chama halali kisheria na kinafanya kazi yake yake kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi" Mjumbe Kamati Kuu CHADEMA na Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Frederick Sumaye.

MY TAKE:

Mjusi ukimkimbiza sana akifika ukingoni ambapo mbele hakuna njia tena, hugeuka nyoka na kuanza kukukimbiza wewe. Siasa CCM wanazofanya hazijawahi kufanikiwa sehemu yoyote Duniani. Kwamba mshindani wako unamfunga mikono kwa nyuma halafu unataka mpande ulingoni kupambana kisha unajisifu umeshinda. Ni kutojitambua na ni aibu.
 
Hess

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
593
671
Sumaye huyu, "... ukitaka mambo yako yafanikiwe njoo CCM" - Naikumbuka kauli hii ya kifedhuri. Acha aumizwe, wametuumiza sana wakiwa upande ule.... simuonei huruma japo yuko upande wetu sasa. What goes around... hata watesi wetu wa sasa kuna muda watakuwa kama Sumaye... Historia ni mwalimu mzuri sana.
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,736
27,801
Utaratibu wa kutembelea miradi ukoje?

Sumaye atambue na kuheshimu mamlaka za nchi...!
 
Chintu

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
5,348
3,362
Sumaye huyu, "... ukitaka mambo yako yafanikiwe njoo CCM" - Naikumbuka kauli hii ya kifedhuri. Acha aumizwe, wametuumiza sana wakiwa upande ule.... simuonei huruma japo yuko upande wetu sasa. What goes around... hata watesi wetu wa sasa kuna muda watakuwa kama Sumaye... Historia ni mwalimu mzuri sana.
Analalamika kadozi kenyewe kadogo tu. Hivi anajua maumivu waliyopitia wapinzani enzi yuko upande wa watesi?
 
MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
26,227
19,581
Chadema haipo juu ya sheria na utaratibu
Hawezi kuingia bila taarifa kwenye ukumbi wa halmashauri wakiwa na sare za chama kisha kufanya vikao!
Walipaswa kufuata utaratibu
Pia Sumaye hana wakumtisha
Aache kutoa hizo kauli za kijinga
 
MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
26,227
19,581
nchi nzima ilani inayotekerezwa ni ya ccm, na ndio waliounda serikali, hata huyo meya anatekereza ilani ya ccm kupitia halmashauri aliyopo. wakwenda kukagua utekerezaji ni ccm na si vinginevyo. huo ndo ukweli.
Kuna utaratibu unatakiwa kufuatwa
Sio kukurupuka tu
 
CAMARADERIE

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
4,423
1,903
Chadema haipo juu ya sheria na utaratibu
Hawezi kuingia bila taarifa kwenye ukumbi wa halmashauri wakiwa na sare za chama kisha kufanya vikao!
Walipaswa kufuata utaratibu
Pia Sumaye hana wakumtisha
Aache kutoa hizo kauli za kijinga

Hapa ni Ikulu na sio Lumumba?

BN649541.jpg
 
Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
11,294
7,985
nchi nzima ilani inayotekerezwa ni ya ccm, na ndio waliounda serikali, hata huyo meya anatekereza ilani ya ccm kupitia halmashauri aliyopo. wakwenda kukagua utekerezaji ni ccm na si vinginevyo. huo ndo ukweli.
Kwenda kukagawa madiwani wanavyotekeleza ilani ya CCM ni kosa?.
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
10,148
16,560
Sumaye ameiomba Serikali iache kuwafanyia fujo CHADEMA. wanayo haki ya kutembelea Sehemu walizoshinda ili kuona kama kweli Madiwani wao wanafanya kazi walizowaahidi wananchi.

Hata kama mie sio mwanasiasa, nakubaliana na Sumaye kwamba serikali sasa imeanza kufanya mambo kwa ujinga na upumbavu. Hii kamata kamata ya viongozi wa upinzani inapita mipaka sasa. Nimeona wakimzuia Meya hapa Dar, na polisi kumsubiri mlangoni mwingine kule Arusha kwa masaa zaidi ya sita wamkamate baada ya kikao.

Huu ni uumbavu na ujinga unaofanywa, naamini, kwa shinikizo la viongozi wa CCM, ambao hautaleta hali nzuri kwa nchi yetu - ukosefu wa amani kwa sababu tu tuna siasa za vyama vingi. Na bado tunashuhudia ujinga mwingine ukiendelea Bungeni.

Kama Magufuli anaona siasa za vyama vingi nchini hazifai, basi tufanye referandum tena kuamua kama turudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Lakini ujinga na upumbavu wa namna hii hauna manufaa hapa nchini.
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,736
27,801
Kwa hiyo polepole anapozunguka hakuna kosa jinga sana wewe

Swissme
Pole Pole ni Chama chenye dola ...1

Pole Pole amezungukia wanaCCM...2

Mkitaka kujilinganisha na polepole mngeshinda uchaguzi .
 
The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
14,137
10,843
nchi nzima ilani inayotekerezwa ni ya ccm, na ndio waliounda serikali, hata huyo meya anatekereza ilani ya ccm kupitia halmashauri aliyopo. wakwenda kukagua utekerezaji ni ccm na si vinginevyo. huo ndo ukweli.
Miaka yote hakukuwa na Ilani .................!!?
 
koban

JF-Expert Member
Oct 29, 2015
249
98
Kama hawataki basi wafute vyama vya upinzani kila maali kamatakamata inakera Sana sasa hii ndio demokrasi gani eti nchi ya amani
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,736
27,801
Hata kama mie sio mwanasiasa, nakubaliana na Sumaye kwamba serikali sasa imeanza kufanya mambo kwa ujinga na upumbavu. Hii kamata kamata ya viongozi wa upinzani inapita mipaka sasa. Nimeona wakimzuia Meya hapa Dar, na polisi kumsubiri mlangoni mwingine kule Arusha kwa masaa zaidi ya sita wamkamate baada ya kikao.

Huu ni uumbavu na ujinga unaofanywa, naamini, kwa shinikizo la viongozi wa CCM, ambao hautaleta hali nzuri kwa nchi yetu - ukosefu wa amani kwa sababu tu tuna siasa za vyama vingi. Na bado tunashuhudia ujinga mwingine ukiendelea Bungeni.

Kama Magufuli anaona siasa za vyama vingi nchini hazifai, basi tufanye referandum tena kuamua kama turudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Lakini ujinga na upumbavu wa namna hii hauna manufaa hapa nchini.
Upumbavu ni kufanya mambo bila kuzingatia sheria ukategemea utaachwa eti kisa una kitambi!

Nimeuliza swali ...utaratibu wa kukagua miradi ukoje?
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,736
27,801
Kama hawataki basi wafute vyama vya upinzani kila maali kamatakamata inakera Sana sasa hii ndio demokrasi gani eti nchi ya amani
Hakuna demokrasia ya kujidai wewe ni mkagua miradi ambayo hujaitolea hela na wala hukuipanga.
 
kagombe

JF-Expert Member
Mar 1, 2015
3,434
1,537
Heshima kwenu wakuu,

Sumaye ameiomba Serikali iache kuwafanyia fujo CHADEMA. wanayo haki ya kutembelea Sehemu walizoshinda ili kuona kama kweli Madiwani wao wanafanya kazi walizowaahidi wananchi.

Hapa Ubungo kuna diwani wa CHADEMA, sisi kama Viongozi wake tumekuja kuona utendaji wake je anafanya kazi kweli au hafanyi. Sasa kosa lipo wapi?

Polepole na Bulembo wa CCM wanazunguka kila Halmashauri nchi wala hawakatazwi na haiwi nongwa. Lakini chadema wakitembelea pale wanapoongozwa wanakamatwa wanatiwa ndani.

Tunaomba Serikali ituache tuwatumikie wale waliotuchagua sababu hii miradi tunayoitembelea sio ya Chadema tu bali itatumiwa na Vyama vyote.

"Tunaomba tu Serikali ituvumilie, CHADEMA ni chama halali kisheria na kinafanya kazi yake yake kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi" Mjumbe Kamati Kuu CHADEMA na Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Frederick Sumaye.

MY TAKE:

Mjusi ukimkimbiza sana akifika ukingoni ambapo mbele hakuna njia tena, hugeuka nyoka na kuanza kukukimbiza wewe. Siasa CCM wanazofanya hazijawahi kufanikiwa sehemu yoyote Duniani. Kwamba mshindani wako unamfunga mikono kwa nyuma halafu unataka mpande ulingoni kupambana kisha unajisifu umeshinda. Ni kutojitambua na ni aibu.
Kawachoma msumari WA motto
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

35 Reactions
Reply
Top Bottom