Sumaye: Serikali itambue CHADEMA ipo kisheria, wasitake vurugu bila sababu

Chadema haipo juu ya sheria na utaratibu
Hawezi kuingia bila taarifa kwenye ukumbi wa halmashauri wakiwa na sare za chama kisha kufanya vikao!
Walipaswa kufuata utaratibu
Pia Sumaye hana wakumtisha
Aache kutoa hizo kauli za kijinga
CCM mna hati miliki ya hii nchi??
 
Sumaye huyu, "... ukitaka mambo yako yafanikiwe njoo CCM" - Naikumbuka kauli hii ya kifedhuri. Acha aumizwe, wametuumiza sana wakiwa upande ule.... simuonei huruma japo yuko upande wetu sasa. What goes around... hata watesi wetu wa sasa kuna muda watakuwa kama Sumaye... Historia ni mwalimu mzuri sana.
kila binadamu hukosea kwa wakati wake ukifika wakati akaona njia hurudi kundini
 
Hivi jamiiforums haiwezi kutengeneza programu ambayo inaweza kutambua pumba na mchele? Kisha ikatumika kwa wanaojibu hoja.
 
Utaratibu wa kutembelea miradi ukoje?

Sumaye atambue na kuheshimu mamlaka za nchi...!
Hizo sheria unazo taka mwenzetu ziheshimiwe zilitungwa kwa ajili ya kuheshimiwa na upinzani pekee?? Maana naoina bulembo anapiga jaramba kila siku huko majimboni na kwenye miradi , acheni ubinafsi unajenga chuki na taifa haliwezi kusonga mbele maana litakuwa na laana ya manung'uniko - hiyo ni kiroho zaidi kwa wanao amini
 
Sumaye huyu, "... ukitaka mambo yako yafanikiwe njoo CCM" - Naikumbuka kauli hii ya kifedhuri. Acha aumizwe, wametuumiza sana wakiwa upande ule.... simuonei huruma japo yuko upande wetu sasa. What goes around... hata watesi wetu wa sasa kuna muda watakuwa kama Sumaye... Historia ni mwalimu mzuri sana.

Nadhani unafanya makosa kwa kutumia nukuu hizi. Akiwa CCM, alikiamini na kujivunia lakini baadae yale mazuri aliyokuwa anayategemea yalikoma. Huko kukoma ndio kumlifanya atafute ubavu mwingine, na kamwe kama ukimsikiliza vizuri hawezi tena kuisemea CCM kivile. Pengine sasa hivi na amedhihirisha kuridhika na sera za Chadema, na ni rahisi kukushauri ujiunge Chadema. Haya makitu yako dynamic yanabadilika. Usidhani CCM ya Nyerere ni sawa na ya Mwinyi, au Magufuli!
 
Kuna utaratibu unatakiwa kufuatwa
Sio kukurupuka tu
Ninacho sangaa zaid ni pale sheria zinapo hitajika zitumie na kundi moja huku lingine likizigeuzia mgongo hiyo ni roho ya ubinafsi na italifanya taifa lisisonge mbele kwa litakuwa ni taifa la manung'uniko mda wote na manung'uniko yakizid sana ni laana kwa taifa - hii ni kiimani zaid kwa wanao amini katika maandiko matakatifu
 
Acheni kubeza kila kitu kinapita tusijione tuko juu zaidi ya kujenga chuki kati ya wafuasi na wafuasi
 
Kila mtu afanye mkutano kwenye eneo lake aliloshinda sio kuzunguka nchi nzima sasahivi ni kufanya kazi na sio muda WA kufanya siasa na pia ilani inayotekelezwa ni ilani ya CCM maana ndio inayoiongoza serikali na ndio iliyoshinda uchaguzi na sio vinginevyo kikubwa tumuunge mkono mheshimiwa Rais katika jitihada za kuletea taifa maendeleo Huyo anayesema kutembelea maeneo walioshinda asipoteze muda inamaana hawawamini waliowaweka kwamba wanaweza kufanya kazi na kama ndo hivyo kuna haja ya wananchi kuwaondoa katika uchaguzi ujao waweke CCM maana ndio wanauhakika na dhamira ya dhati ya kuletea taiga hili maendeleo
 
Upumbavu ni kufanya mambo bila kuzingatia sheria ukategemea utaachwa eti kisa una kitambi!

Nimeuliza swali ...utaratibu wa kukagua miradi ukoje?

Mkuu kama kweli una nia njema, basi swali lako linapaswa kuwa "utaratibu wa kukagua miradi kwa viongozi wa vyama vya upinzani ukoje?"

Maana hatutarajii kwamba huo utaratibu unapaswa kufuatwa na viongozi wa upinzani peke yake.
 
nchi nzima ilani inayotekerezwa ni ya ccm, na ndio waliounda serikali, hata huyo meya anatekereza ilani ya ccm kupitia halmashauri aliyopo. wakwenda kukagua utekerezaji ni ccm na si vinginevyo. huo ndo ukweli.
Huo sio ukweli ila ni uchochezi
 
Tatizo Hawa ccm wanapataga ufahamu wakihamia kwingine.

Tunakumbuka na yeye aliwatumia Hawa jamaa ,mwembechai na kusongesha mbwa msikitin akiwa anajua kabisa kuwa anawakwaza watu.
 
Mkuu kama kweli una nia njema, basi swali lako linapaswa kuwa "utaratibu wa kukagua miradi kwa viongozi wa vyama vya upinzani ukoje?"

Maana hatutarajii kwamba huo utaratibu unapaswa kufuatwa na viongozi wa upinzani peke yake.
Utaongeleaje Subset?
Halmashauri ina kamati kadhaa ambazo huwa zina ratiba za ukaguzi wa miradi.

Msitake kufanya Maigizo na kujidai nyie ndio CCM.Waliopewa dhamana ya kuongoza dola ni CCM...

By the way kila mtu akiamua kujikagulia miradi patakalika?

Kwa nini Mkurugenzi ambaye ndiye msimamizi wa miradi hakuhusishwa?wakati wa ukaguzi mlikuwa mnamuuliza nani?
 
Chadema haipo juu ya sheria na utaratibu
Hawezi kuingia bila taarifa kwenye ukumbi wa halmashauri wakiwa na sare za chama kisha kufanya vikao!
Walipaswa kufuata utaratibu
Pia Sumaye hana wakumtisha
Aache kutoa hizo kauli za kijinga
Ukumbi wa Halmashauri unamilikiwa na mkuu wa Wilaya? huu ujinga wa kiwango cha makinikia
 
Hata kama ni Huyo meya unayesema ni kwamba halmashauri zote nchini zipo wizara ya TAMISEMI inayoongozwa na waziri WA CCM tunarudi palepale kwamba ilani inayotekelezwa ni ya CCM na sio vinginevyo
 
Sumaye huyu, "... ukitaka mambo yako yafanikiwe njoo CCM" - Naikumbuka kauli hii ya kifedhuri. Acha aumizwe, wametuumiza sana wakiwa upande ule.... simuonei huruma japo yuko upande wetu sasa. What goes around... hata watesi wetu wa sasa kuna muda watakuwa kama Sumaye... Historia ni mwalimu mzuri sana.
Mtu akitubu husamehewa,kama kaja upande wa pil na anapigania haki si vibaya,tumuunge mkono,maana chama si Baba eti hauwez kukikana endapo kinaenda tofaut au ukitambua hakitendei Wananch haki ulioiona ni haki yao,mkuu asilimia kubwa Mtu akiwa Ccm uelewa humtoka,na ni wachache wanaojitambua mfano ni Bashe na Deo Filikunjombe ambaye kwa sasa hatuko naye tena Dunian,Mungu amrehemu,fikra zake tunazikumbuka mpk leo
 
Sumaye amezungumza kwa hekima sana, kama watawala wana masikio watasikia.

Watawala ni vema watambue kuwa wananchi sio wajinga, viziwi wala vipofu, Watanzania wengi sio wanacha wa vyama vya siasa. Wengine wakati wa uchaguzi 2015 tulipigia kura zaidi ya chama kimoja, kwa hiyo ingependeza kama kura na uamuzi wa wananchi vikaheshimiwa.

Vv
 
Kwa hiyo polepole anapozunguka hakuna kosa jinga sana wewe

Swissme
Ana kosa tena kosa kubwa sana maana utaratibu huu ulikuwepo enzi zile chama kimeshika hatamu ya uongozi lakini since 1992 mfumo wa vyama vingi ulipoingia ukaja utaratibu mwingine wa namna serikali inavyofanya kazi ila CCM huwa wanajitoa ufahamu hasa hapa mwisho mwisho wa awamu ya nne na matokeo yake na wapinzani nao wakaona ni wakati muafaka kufanya yao lakini tofauti na matarijio yao serikali ikaingilia kati.

Kuna haja ya taratibu kufuatwa kwa pande zote chama tawala na upinzani kuhakikisha shughuli zinatekelezwa na ndio maana kuna kamati za siasa za vyama ambazo majukumu yake ni kupokea taarifa ya shughuli zilizotekelezwa na kutoa mapendekezo ili madiwani wao wakiongozwa na Meya wafanyie kazi lakini kwa Tanzania haijulikani kazi ya chama cha siasa ni zipi na serikali ni zipi.....na ndio maana nakumbuka hata kina Nape na Kinana waliwahi kumchukua Balozi wa China kwenda kukagua miradi ya maendeleo sema zile kelele za wananchi ikabidi Membe atoe tamko / katazo kwa kuwahusisha mabalozi kwenye shughuli za kichama.
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom