TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Huku kutapatapa kuwa Magufuli aliuza nyumba za Serikali sasa wamuulize Sumaye si wanaye huko, atawafafanulia. Wamuache Tingatinga achanje Mbuga.
Wakati suala la kuuzwa kwa nyumba za serikali likileta utata bungeni, wabunge wa CCMwakitaka lisijadiliwe huku wale wa upinzani wakilazimisha na kuliibua, katika fukunyuku zangu ni kuwa hili suala lilipata baraka zote na serikali ya kipindi hicho [awamu ya 3].
Akihojiwa na mwandishi wa habari ambaye sasa ni mbunge Saed Kubenea, waziri mkuu mstaafu aliyejiunga na upinzani alisema kuwa uuzwaji wa nyumba hizo ulifanywa kwa kuwa zilikuwa nyingi mno na serikali kushindwa kuzi 'maintain' katika ubora unaopaswa, na ulipata baraka za serikali na hakukuwa na mizengwe wala ufisadi wa aina yoyote.
Wakati huohuo
Nikiwa kwenye maktaba yangu nikapitia habari kutoka gazeti kubwa linaloaminika la Mwananchi likionyesha kuwa mheshimiwa rais wa sasa hivi John Pombe Magufuli sio msafi kivile,na msimamia ukweli daima kama watanzania wengi walivyoaminishwa na kumnadi bali na yeye pia ni fisadi au 'jipu'
Licha ya kuandamwa na kashfa kadhaa ikiwemo ya kununua kivuko kibovu cha Dar-Bagamoyo, na kuwa na reputation kufanya maamuzi mengi yasiyozingatia technicality na maono ya mbali hivyo kuisababshia serikali hasara na kuleta mtafaruku mkubwa kwa umma.
Kwenye gazeti hili inataarifiwa kuwa ukaguzi wa CAG katika kipindi cha mwaka 2O1O/2O11 na 2O11/12 umebaini kuwa mheshimiwa huyu kipindi hicho akiwa waziri wa ujenzi bungeni Novemba 2O13 alitoa taarifa za uongo kuhusu fedha zilizotumika kwenye miradi ya barabara.
View attachment 349089