Maofisa wa Sumatra nawaomba mfanye utafiti/uchunguzi nyakati za asubuhi pindi mabasi ya mikoani yanapo anza safari zake kuelekea mikoani, kituo kidogo cha kibamba CCM ambacho kimeonekana kuwa na idadi kubwa ya abiria wanao pandia hapo hivyo kusababisha vurugu na msongamano wa mabasi kiasi cha kuhatarisha usalama wa abiria na vyombo vyenyewe. Baadhi ya mabasi hulazimika kusimama katikati ya barabara na kupandisha abiria jambo hilo ni hatari sana!! Fanyeni uchunguzi kuanzia saa 12 asubuhi
Kwa wakati huu Sumatra inaweza kufanya jambo moja kwa muda huu nalo ni kufanya upanuzi wa kituo hicho ili kuepusha hatari inayo weza kutokea, tusisubirie ajali mbaya itokee ndipo tuchukue hatua.
Taadhari kabla ya hatari!!