Malilambwiga
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 485
- 296
Kwa miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la ujangiri ktk hifadhi zetu na tembo pamoja na faru ni wanyama ambao wamekuwa wakilengwa kutokana na oembe/meno yao kutumika kama vipusa vya mapambo duniani.
Mara zote serikali imekuwa ikilaani au kutoa matamko yasiyozaa matunda ya kuwalinda wanyama hao.
Kutokana na kushamiri kwa ujangiri imefikia hatua wananchi kuwanyooshea vidole baadhi ya viongozi wa chama tawala na serikali kuhusika na uhalifu huo.
Kitendo cha kutunguliwa Helkopta na majangiri kunathibitisha kuwa majangiri wamejipanga kwa vifaa na mbinu kuliko askari wa wanyama pori.
Suluhisho pekee la uhalifu huu ni kuwanyang'anya wananchi wote wanaomiliki silaha zenye uwezo wa kuua mnyama na wabakie wale wanaomiliki bastola pekee.
Aidha serikali iweke utaratibu wa mmiliki wa silaha anapohitaji kununua risasi aeleze matumizi ya risasi za awali alizitumiaje.
Nchi hii ni ya amani na hivyo haiingii akilini watu kumiliki silaha kwa kiwango kikubwa huku hakuna anateulizwa juu ya matumizi ya silaha hizo mwaka hadi mwaka.
Wakati haya yakiendelea serikali ipige marufuku watu kumilikishwa silaha kwani uzoefu uneonyesha hata wanaozimiliki wakati mwingine huzikodisha kwa wahalifu.
Njia ya pekee ya kunusuru wanyama wetu kwa kizazi kijacho ni kunyang'anya watu wote wanaomiliki silaha aina ya Rifle na Mark four badala yake raia aruhusiwe kumiliki bastola tu kwa ajili ya kujilinda na si vinginevyo.
Serikali ikiacha kuchukua hatua hizi na tukaendelea na mfumo tulionao tutarajie sisi watanzania kuwa watalii miaka ijayo kwenda kuwaona wanyama wetu nje wanaobebwa na ndege za Katar.