Ngoja nimtolee povu kidogo mbunge wangu bwege
binafsi siungi mkono hoja kuwa mbunge makini ni yule anaelialia kuulizia maendeleo ya jimbo lake wakati kila bunge la bajiti linapitisha pesa za maendeleo kwa kila jimbo
Ndio maana huoni mawaziri wakitetea jimbo lakini maendeleo kwao yanapatikana......... si wkasababu yeye ni waziri au kwa kuwa harususiwi kusimama kama mbuge.
Ngoja nikuulize tena wabunge makini kwanini hawasimami na kuanza kuulizia maji ja zahanati majimboni mwao mfano Mbowe, Zitto.
kwa muono wangu pesa kwa ajili ya miradi ya maendeleo huwa zishatengwa na ni kazi ya mbunge kufatilia kwa wizarani na kwa katibu mkuu na hazina ili kujua kama zishapelekwa au laa, na kama bado hapo humshinikiza waziri apeleke ndani ya muda, na ndio maana utaona baadhi wa wabunge huamia dsm kumghasi waziri aachie pesa. Na ndio maana mawaziri na wabunge makini husikii wakilalamika kama wengine ndani ya bunge. pale ni sehemu ya kueleza matatizo ya taifa....
Ngoja nikupe mambo 2 kama maono wangu kuhusu bwege na kilwa.
1. bwege huwa anaishi kilwa kwa sabaubu ili uwe mbunge kilwa wanakilwa nanataka nawe ukaishi kule kule na ndio silka ya watanzania.
bwege s tu kwanmba haji kwa kufatilia pesa za jiboni kwake bali anaogopa na hajui kuongea mwele ya watu makini bali yeye husikiliza tu.
2. wilaya ya kilwa ni miongoni mwa wilaya zilizobarikiwa na kutokana na gesi hupokea service leavy zaidi ya milioni 100 kwa mwezi.
Je wananchi wananufaika vp na pesa hiyo.?
Kigoma ambapo mbunge wake halii lii kuhusu bajeti ya maendeleo ya wilaya/jimboni kwake nao ni ktk wilaya yenye vyanzo hafifu vya mapato mara 100 ya kilwa. lakini ni wilaya pekee inayosomesha bure wanafunzi kwa form v na vi.
Pato wanalotegemea kusomeashea inatokana na makusanyo ya levy inayotokana na minara yasimu tu.
Zitto Kabwe: Tunasomesha wanafunzi wa Kigoma Ujiji kidato cha 5 & 6 popote walipo nchini
Kilwa ina minara ya simu mingi tu achilia pato kutokana na gesi, hivyo kilwa ina uwezo wa kusomesha hadi chuo kikuu ingeamua. badala yake mnatulamba visogona kutufanya matumbili wote kwa mh wetu FUTUHI.
Ye yupo yupo tu yupo yupo tu kwa ajili ya kuchekesha watu na ukweli ni kuwa hata watumishi wa halmashauri wanamwombea aendeleeee kuwa mbunge ili wapate kutafuna vizuri pesa za wananchi
VIJIMAMBO: Wizi wa kufuru fedha za gesi
Kwa kumalizia niseme tu kilwa haiitaji masifi ccm na futuhi kilwa inahitaji muono mpya
MAJIRA - GAZETI HURU LA KILA SIKU:: Halmashauri Kilwa yakumbwa na ufisadi
Niishie hapo kwa sasa.