Sudan yapunguza wanajeshi wake nchini Yemen

Sudan yapunguza wanajeshi wake nchini Yemen

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,599
Waziri Mkuu wa Sudan: Tumepunguza askari wetu Yemen, tumebakisha wanajeshi elfu tano

Dec 09, 2019 12:23 UTC

[https://media]

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok amesema, nchi yake imepunguza idadi ya askari wake walioko nchini Yemen kutoka 15,000 hadi 5,000 na kuthibitisha punguzo hilo la askari hao katika mgogoro ambao amesema hauwezi kutatuliwa kijeshi.

Hamdok, ambaye anaongoza serikali ya kiraia ya Sudan iliyoundwa mwezi Septemba kupitia makubaliano na jeshi ya kugawana madaraka baada ya kumuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir, ametoa ufafanuzi hadharani kwa mara ya kwanza kuhusu idadi halisi ya askari wa Sudan walioko vitani nchini Yemen.

Waziri Mkuu wa Sudan ameyasema hayo baada ya kurejea nchini humo kutoka safarini nchini Marekani.

Amewaeleza waandishi wa habari mara baada ya kuwasili mjini Khartoum: "Kuhusu Yemen tumesema kuwa hakuna ufumbuzi wa kijeshi na lazima lipatikane suluhisho la kisiasa."

[https://media]Askari wa Sudan waliopelekwa vitani nchini Yemen

Askari wa Sudan walitumwa nchini Yemen kama sehemu ya muungano vamizi wa kijeshi ulioundwa na Saudi Arabia, ambao ulianzisha hujuma na mashambulio ya kijeshi dhidi ya nchi hiyo masikini ya Kirabu mwezi Machi 2015.

Uamuzi wa serikali ya Sudan ya enzi za Omar al-Bashir wa kutuma wanajeshi wake katika uvamizi wa kijeshi dhidi ya Yemen ulilaaniwa vikali na makundi mbali mbali ya kisiasa nchini Sudan.

Hayo yanajiri huku duru kadhaa zikiripoti kuwa, tangu mwezi Sepetmba, Saudia imekuwa ikifanya mazungumzo yasiyo rasmi ya usitishaji vita na harakati ya Ansarullah ya Yemen. Uamuzi huo wa utawala wa Aal Saud umechukuliwa kwa lengo la kutafuta njia ya kujitoa kwenye vita vilivyoifedhehesha Riyadh, baada ya mshirika wake mkuu katika muungano huo vamizi wa kijeshi, yaani Imarati kuamua kuondoa askari wake nchini humo.../
 
Wasaudia Vita hawawezi! Wao ni wavaa vilemba na Wala tende wazoefu..
Hata silaha Wanazonunua kutoka USA hawajui na hawatajua kuzitumia..wiki Jana helicopter yao ilidunguliwa na houth rebels, siyo hivyo tu drones na aina nyingine ya aircraft Kama rumous ya miezi minne iliyopita kwamba houth walidondosha Saudis f 16..
So hivyo tu ardhini wameendelea kupigika ipasavyo miezi kadhaa iliyopita walikimbia kifaru hatari zaidi duniani kutoka marekani ( Abram m1)
Licha ya hayo pilot wengi was ndege zao za kivita ni wapakistani..
 
Saudia hii vita imemshinda na anaanza kutengwa na washirika wake

Back
Top Bottom