SUDAN KUSINI haikuwa tayari kujiunga EAC

Andrew123

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
7,052
8,638
Tukitizama figisu figisu za hawa jamaa zetu tuliowakaribisha majuzi kwenye jumuiya yetu pendwa ya EAC, nadhani hatukupaswa kuwakaribisha kwa sasa maana bado wanaendeleza sarakasi zao za kuteuana na kumwagana (hasa nafasi ya Makamu wa Rais).

Hawa jamaa ni kama hawaelewi dunia inaendaje. Na mateso wanayopata raia wao kwenye kambi za wakimbizi. Sasa Machar kapigwa chini kateuliwa mwingine duuh! tujiandae kupokea wakimbiz kwa wingi toka huko.

NB:
Hivi hakuna namna ya kusitisha uanachama wao EAC tukawakaribisha kina Koffi Olamide? au hata Wahabeshi toka Ethiopia?
 
Hao Ma-niga toka huko sudani ni watata hata kwa kuwaangalia tu. Sijui ilikuaje wakakaribishwa kwenye jumuiya kiulaini hivyo bila kupitia hali ya usalama kwao. Hapa tumelivagaa ZIGO la NNYA maana kuwamwaga si rahisi tena!
 
Mtashangaa Somalia nayo itakaribishwa ndio mtajua hiyo EAC ni upuuzi mtupu.
 
kiukwel tuseme tuliwakaribisha kichwa kichwa hawa jamaa zetu. Sioni la kufaidisha jumuiya toka kwa hawa wandugu
 
Pale Museveni katupandisha kenga yeye ndio alikomaa waingizwe ili wamsaidie kujenga bomba la mafuta
 
East Afrika ni upuuzi mtupu, genge la kuminya demokrasia kila rais mbabe nchini mwake anatafuta upenyo wa kumiliki East Afrika ikiwezekana Afrika nzima, ndio maana hata juzi wameshindwa kupata mwenyekiti mpya, genge la walafi wa madaraka. Wataunganisha weee, kila nchi ila siku wanaweka rais mmoja kwenye huu muungano ndio hapo tutazalisha wakimbizi kuliko bara lolote lile. Ubinafsi tu hakuna maendeleo wala nini.
 
Iangaliwe namna ya kuwatoa hawa jamaa asee maana naona wao wamezoa vita tu
 
tusubirie mazungumzo mengine ya amani pale Arusha, hope wenye mahoteli watafanya biashara kubwa tu kwa kupokea wageni wa kimataifa toka pande zote za dunia kuja kusuluhisha.
 
Back
Top Bottom