Suala la Yanga kutotaka kucheza tarehe 3 julai ni dharau kwa TFF, serikali na wapenzi wa soka

Nimeona msemaji wa Yanga anayejulikana kama Bumbuli, akitaja mechi zilizobaki katika premier kuwa ni nne tu huku alisema wao yanga hawatambui mechi ya tarehe 3.

Jambo hili kama kweli litatokea, itakuwa ni dharau kwa TFF, serikali ambayo waziri wake alishiriki kwenye kuahirishwa kwa mechi ile na alishiriki kikao cha usuluhishi, pia ni dharau kwa wapenzi wa soka ambao walianza kurudisha mapenzi na soka la nchi hii. Na ninaamini hata mdhamini wa ligi hawezi kufurahishwa na tabia hii wanayotaka kuonesha yanga,ijapo mpaka sasa hivi naamini ni mbinu ya kumzubaisha mpinzani ili a relax halafu siku hiyo imshitukize kama mwivi.

Natoa rai kuwa sasa ndio muda sahihi kwa TFF kuwachukulia hatua kali .wote wanaoendekeza uswahili
Unawalaumu Yanga SC bila kufikiria shida iko wapi...

Tujifunze kuheshimu sheria na kanuni tulizojiwekea wenyewe...

Kosa ni la TFF kwa kukubali kutumiwa na wanasiasa kuharibu mchezo huo...

Mimi nakubaliana na Yanga SC kwa msimamo wao ili wawafundishe TFF kuelewa namna njema ya kuuendesha na kuusimamia soka la Tanzania...

TFF waache ubababishaji. Waende wakacheze wao na Waziri aliyeshiriki hicho kikao...
 
Hili kosa la kuahirisha mechi sio la TFF , ni la serikali, sasa yanga wakidinda sio kwamba wanamkazia TFF wanaikazia pia serikali ambayo ina namna mia za kuwafunza adabu na kuwarudisha kwenye mstari.

Waziri au katibu mkuu au yeyote aliyetoa hili boko hatakubali dharau na aibu zaidi. Sasa kama yanga wanafikiri kusimamia sheria siku zote ndio kunaleta ushindi hawazijui siasa za Afrika. Habe tusubiri kidogo tuone!!

Si rahisi hivyo kama unavyofikiri...

Hata serikali yenyewe inajua kosa liko wapi. Kamwe Yanga SC hawana kosa na kwa hiyo hakuna "base" ya kuwachukulia hatua iwe toka TFF au Serikali in general...

Ili serikali iichukulie hatua Yanga SC ni lazima vivyo hivyo itazame sheria na kanuni za Ligi na soka kwa jumla...

Kote huko, Yanga hawana kosa....!!
 
Wawafundishe mara ngapi?Si walishakimbia mechi ya awali?Kwa hiyo unataka migogoro hii iendelee kwa kuzalisha mgogoro mwingine?

Fikiria hawa yanga wakigomea mechi unadhani watapewa wao pointi 3 ?
Na wakipewa Simba halafu yanga wakaenda CAS huoni ni kuzidi kuleta sintofahamu?Halafu unapowakomoa TFF unataka nini kitokee?Au unadhani watakuwa malaika?
Unawalaumu Yanga SC bila kufikiria shida iko wapi...

Tujifunze kuheshimu sheria na kanuni tulizojiwekea wenyewe...

Kosa ni la TFF kwa kukubali kutumiwa na wanasiasa kuharibu mchezo huo...

Mimi nakubaliana na Yanga SC kwa msimamo wao ili wawafundishe TFF kuelewa namna njema ya kuuendesha na kuusimamia soka la Tanzania...

TFF waache ubababishaji. Waende wakacheze wao na Waziri aliyeshiriki hicho kikao...
 
Kwani mpira wa miguu ili ukamilike ni mambo gani ya kuzingatia? Je kamisaa wa mchezo walikuwepo? Referii je, hawa Yanga nani aliwakagua tayari kwa kuanza mechi katika hizo dk za 30? Wanaweza wakawa na hoja ila kwa stail hii wataanguka mapema.
Kwanini hawakufika kosa ni la nani?
 
Si rahisi hivyo kama unavyofikiri...

Hata serikali yenyewe inajua kosa liko wapi. Kamwe Yanga SC hawana kosa na kwa hiyo hakuna "base" ya kuwachukulia hatua iwe toka TFF au Serikali in general...

Ili serikali iichukulie hatua Yanga SC ni lazima vivyo hivyo itazame sheria na kanuni za Ligi na soka kwa jumla...

Kote huko, Yanga hawana kosa....!!
Kuwa na kosa au kutokuwa na kosa hakutakuwa sababu kuu ya kuitia adabu yanga. Ile jeuri Yanga inataka kuonyesha kwa sababu tu iko kwenye kanuni ndio itakayowakera hao waendesha nchi kiasi cha kutaka kutoa somo. Kwanza wanaweza wakaiacha Yanga i get away hata na hili swala ili wajione wameshinda. Halafu ndio waundiwe zengwe, fitina, fitina ya kuangusha ufalme. Fitina tena iliyo ndani ya kanuni hizo hizo, Uone kama watachomoka. Nchi hii hii watu wanapewa kesi za uhujumu uchumi, baba na mwana kubaka na madawa ya kulevya na wenye mamlaka na hawatoki. Yaani wao ndio judge,jury and executioner, acha kabisa. Mkubwa hakosei. Na Mwalimu akiamua kulitafuta kosa kwa mwanafunzi halikosi.Yanga anzeni, halafu wenye mamlaka watajibu, na wanavisasi sana hao!
 
FIFA hairuhusu serikali kuingilia mpira kama itatokea hivyo kuna janga lina kuja kwenye mpira wa bongo
Hata serikali inajua vizuri jambo hilo, ila ina namna na hila nyingi. Serikali iliwekeza kwenye maridhiano ya kiafrika kupeleka mambo mbele. Sasa kuna watu wanataka kwenda na kanuni tu. Na hawajui sheria ni msumeno na wao ndio wameshika kwenye makali. Matokeo yake, Baadae kidogo hakutakuwa na mswalia mtume, ni rungu na panga tu. Kama Yanga wako perfect sana kikanuni basi acha waendelee kuwa wa kwanza kurusha jiwe.
 
Back
Top Bottom