Suala la mchanga wa dhahabu Rais Magufuli usitetereke

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Sep 18, 2013
9,125
8,644
Kwa mara ya kwanza najitokeza kukuunga mkono raisi Magufuli kwa kukataza kusafirishwa nje ya nchi mchanga ulio na madini mbalimbali hususani dhahabu.
Nimewahi kuchimba na kufanya kazi hapo mgodini Bulyanhulu pia nimeishi karibu kabisa na machimbo madogo madogo ya dhahabu kama yale ya Bolyanholo (Bulyanhulu zamani yakiitwa Bariadi kutokana na wingi wa wanantuzu kutoka maeneo ya Bariadi.

TUKIO LA KUIBWA KWA MCHANGA NJIANI

Ni tukio lililotokea miaka michache iliyopita likiwahusisha Makota (wanunuzi wa dhahabu) na madreva wa malori (makontena) ya mchanga kuyatoa mgodini na kuyapeleka bandarini) tayari kwa kusafirishwa kwenda japani. Siku hiyo kama kawaida yao (makota) ya kununua mchanga wakimtumia (jina nalihifadhi) ambaye alikuwa ni mtaalamu wa kufungua seal za makontena na kurudishia kama vile halijafunguliwa, walipata taarifa kutoka kwa wahusika (wapiga dili wa ndani ya mgodi) kuwa katika kontena zaidi ya 20 kuna mbili hazikupitishwa process plant (hazijachejuliwa dhahabu) hivyo zina concentration kubwa ya dhahabu hivyo wakae mkao wa kuzipakua zote na kujaza udongo hewa pamoja na samandi ile nyeusi nzito. Baada ya kufika sehemu husika kuliibuka ugomvi baina yao wa kugombea kontena hizo huku wakitishiana kuuana na kuzidiana pesa. Baadae kundi moja lilipokosa mzigo likaamua kutoa taarifa zilizowezesha kukamatwa kwa wahusika na kesi ikasikilizwa ambapo wengi wao walihukumiwa kwenda jela. (wawili ninaowafahamu mimi nilijulishwa wako Kakola baada ya kumaliza kifungo.

Lengo la kuandika huu uzi ni baada ya kujulishwa kuwa kikozi kazi cha mheshimiwa Magufuli kimeshafika maeneo ya Bulyanhulu wakiwemo wanaovuga kuwa ni waandishi wa habari na nimefurahi katika walioomba kutoa ushuhuda ni mmoja wa walihukumiwa kufungwa kwa wizi wa mchanga.
Nakumbuka alishawahi kusema kuwa kipindi wanaiba huo mchanga wa dhahabu, mfuko mmoja wa kilo 25 (ule wa cement) walikuwa wanatoa 230gm za dhahabu.
Anyway tusubiri hao waandishi wapelelezi kama kweli watatoa taarifa sahihi japo na mimi kama ningelikuwa karibu, hakika ningeomba kuhojiwa nami ninayo ya kusema faragha.
 
Back
Top Bottom