Suala la Madini: Sielewi mwalimu Nyerere alikusudia nini hasa...

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,735
"Madini sio nyanya kwamba yataoza wayaache kwa ajili ya kizazi kijacho" J.K Nyerere...

Hii ni moja ya kauli inayoishi kutoka kwa Mwalimu Nyerere.

Alimaanisha nini?
1: Watanzania Tusomee Sheria na Tutafute exposure duniani katika madini ili kizazi hicho alichodhani anawatunzia madini kiweze kuwa na uwezo ulioshiba wa Kuingia Mikataba na kupitisha sheria?

2:Watanzania Tusomee madini, Ili siku moja tuje tumiliki migodi yetu sisi wenyewe, Ili tuwe na ujasiri wa kusema "Tanzania ni nchi Tajiri"?

3:Ni kizazi Kipi hasa Mwalimu nyerere alikikusudia aliposema "KIZAZI KIJACHO", Je cha miaka ya 90,Miaka ya 2000,miaka ya 2010+ au kizazi cha miaka ya 2050+

4: Au alikuwa anamaanisha tuwekeze kwenye Uchumi maarifa "Knowledge Economy" ili tuwe na uwezo wa kusimamia rasilimali zetu bila kujali tunachimba sisi,wanachimba wawekezaji kwa ufupi tanzania iwe na watu wenye akili na uwezo mkubwa wa kuamua maamuzi chanya juu ya mali walizonazo bila kujali dunia inabadilika vipi?


wajuvi na watu ambao mmekuwa karibu sana na mazungumzo ya Mwalimu mnaweza kusaidia hapa. Kuna hatari vizazi vikapita bila kujua Jukumu waliloachiwa na wazee wao...
 
Back
Top Bottom