twahil
JF-Expert Member
- May 31, 2011
- 4,100
- 2,793
Salaam wana bodi,
Tangu Mheshimiwa Tundu Lissu adhuriwe huko Dodoma na hatimaye kupelekwa Mjini Nairobi-Kenya, kumekuwepo na mijadala, mivutano na malumbano mengi sana juu ya namna suala hili linavyoshughulikiwa.
Kwa siku za hivi karibuni CHADEMA imekuwa ikiongeza kasi ya kuhamasisha watanzania kuchangia matibabu ya Mheshimiwa Lissu huko Nairobi. Sababu ambazo zimekuwa zikitolewa ni kuwa gharama za matibabu ni kubwa kwani kwa siku ni takribani Milioni 10 za kitanzania. Mchungaji Msigwa wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha Azam alisema kuwa jumla ya Shilingi Milioni 150 zimekwishatumika na bado fedha nyingi zinahitajika.
Kwa hakika matibabu ya Mheshimiwa Lissu yataendelea kutafuna fedha nyingi na kwa kutegemea kupitisha bakuli la michango kila siku kwa watanzania haitawezekana. Sasa kwakuwa Serikali kupitia Waziri wa Afya Ummy Mwalimu imetoa tamko lake kuwa inayo nia ya dhati kabisa kugharamia matibabu ya Mheshimiwa Lissu, basi ni vema Serikali ikaachwa igharamie matibabu hayo na familia yake ichukue jukumu la kuwa msemaji na "role" ya wanasiasa wenzake wa CHADEMA walioko huko Nairobi ipungue kwa wao kuacha kutoa matamko ambayo bado hayamsaidii mgonjwa zaidi ya kumuweka katika "position" ya kutokuwa na uhakika wa matibabu yake kutokana na makusanyo ya fedha za matibabu kuwa "unpredictable".
Ni wakati sasa familia ndio iwe msemaji wa matibabu ya Lissu na familia ndio iwe na maamuzi na sio hawa wanasiasa ambao kwao ni kuona suala la Lissu linatumiwa kukipa umaarufu chama chao.