Simon Templar
Member
- Mar 3, 2016
- 18
- 21
Wakuu,
Tangu kutumbuliwa kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga, Mei 20, 2016 na Mhe. Rais John Magufuli kwa madai ya kuingia Bungeni akiwa 'amelamba kinywaji', kumekuwa na mivutano mingi ya kisiasa kuanzia huko Bungeni hadi jimboni Misungwi.
Kuna kundi la madiwa 19 ambao walikuwepo mjini Dodoma hata wakati Kitwanga anavuliwa koti la uwaziri, ambao tangu wakati huo wameendelea kutetea kwamba mbunge huyo wa Misungwi alionewa, hakulewa, na kulikuwa na njama zilizosukwa na baadhi ya watu hata kabla ya 'kutumbuliwa' kwake.
Wanasema kwamba, ni bahati kwa sababu alivuliwa uwaziri kabla, vinginevyo 'yangeweza kumpata makubwa zaidi ya hayo'.
Wanasema, kuna kundi la mawaziri, wabunge na wafanyabiashara ambao walikuwa nyuma ya mpango huo mbovu na hatari.
Madiwani hawa wametoa matamko mengi kwa vyombo vya habari, lakini ninaona kwamba, kwa kadiri siku znavyosonga, kama wanachokisema ni kweli, basi kuna hatari pengine hata ndani ya CCM kuwa kuna mpango usiofaa.
Na kama wanachosema siyo kweli (rejea hapa), basi nadhani hali siyo nzuri.
Siwezi kujua ni nini na ndiyo maana ninaleta mjadala hapa, lakini kwa hisia za haraka haraka, mtu unaweza kusema kwamba, huenda Kitwanga hakuwa chaguo la 'mtandao' kupata uwaziri wa mambo ya ndani, au wakati akiwa waziri, 'aliingilia rasilimali na vitegauchumi vya watu' wakiwemo wenye 'nasaba' na CCM.
Jana Ijumaa, huko Mwanza, walitoa tamko jingine ambalo sasa linaonyesha kwamba kuna harakati zinazosukwa na baadhi ya vigogo wa CCM 'kumwajibisha' Kitwanga, ambapo sasa wanakwenda jimboni kwake.
Ninalibandika tamko hilo la madiwani hao hapa chini, lakini kwa kuzingatia maadili, nitahariri majina ya wahusika waliotajwa moja kwa moja kwa kuwa naamini Jamii Forums ni jukwaa la habari na linazingatia misingi na sheria zilizowekwa - za kitaifa na kimataifa na maadili ya habari kwa ujumla.
Kila palipo na majina ya watu au taasisi zimewekewa mabano (...) kwa nia njema ya kitaaluma, hasa kwa vile haya ni madai!
===
Maoni yangu:
- Kuna haja ya wahusika ndani ya CCM - kwa sababu Kitwanga ni mbunge na kada wa chama hicho na madiwani hao ni wa CCM pia - kulichunguza suala hilo kwa sababu inaleta picha hasi sana kusikia mnyukano huo kila siku.
- Kwamba kuna njama zinafanywa na baadhi ya vigogo wa chama wakiwemo mawaziri na wabunge, ifahamike, au kama Kitwanga anatumia hiyo kama shield (ngao) kwa yaliyompata, ifahamike pia.
Nawasilisha wadau.
Ndugu watanzania na ndugu waandishi wa habari,habari za mchana huu,Kama mtakumbuka siku kadhaa sisi madiwani 46 wa jimbo wa Misungwi pamoja na wananchi wa kawaida 15 tulikuwa Dodoma kwa mwaliko wa mbunge wa Misungwi Charles Kitwanga ambaye tulishuhudia akivuliwa uongozi kwa sababu ambazo hatukukubaliana nazo kwa kuwa tuliambatana naye pale Dodoma kwa mambo mbalimbali,hatuna sababu za kurudia yale tuliyoyasema.
Ndugu waandishi wa habari Tunapenda tu kuwapa taarifa kwamba kuna baadhi ya madiwani wenzetu 19 wa jimbo la Misungwi waliitwa Mwanza na (kigogo wa CCM Mkoa wa Mwanza) na baadaye akawapa nauli waende Misungwi kwa sababu ambazo baadhi yetu tulizikataa kwa kuwa alituita ili tukazungumzie mbunge wa Misungwi Mhe Charles Kitwanga kwa ahadi kwamba atatupatia pesa iwapo tutakanusha taarifa ambazo tulikuwa tunazitoa kwa vyombo vya habari.
Tunasisitiza kwamba kamwe hatutamsaliti mbunge wetu kwa kuwa sisi na yeye tumechaguliwa na wananchi kwa hivyo lazima tusimamie ukweli na kuweka siasa pembeni.
Katika madiwani kumi na tisa (19) waliokwenda Misungwi kwa kuitikia wito wa (kigogo wa CCM Mwanza) waliokuwa Dodoma walikuwa madiwani sita (6) ambapo wote amewakabidhi kiasi cha shilingi laki moja kila mmoja.
Ndugu waandishi wa habari tunajua siasa za mkoa wa mwanza na mwenyekiti wetu kwa kutumia nafasi yake amekuwa anampinga mbunge wa misungwi na amekuwa mmojawapo anayetumia tatizo la mhe Charles Kitwanga kulikuza na kuliendeleza kwa sababu anazozijua yeye.
Mtakumbuka kwamba chama cha mapinduzi kupitia msemaji wake Christopher Ole sendeka aliishazungumzia kuhusu suala la mhe Kitwanga na akatoa majibu sahihi kwa waandishi wa habari,lakini antony Diallo analazimisha kuliweka lionekane kama ni tatizo kubwa.
(Kigogo huyu wa CCM Mwanza) leo amewaita wanahabari na kuwapa nauli yeye mwenyewe waende Misungwi wakamtukane mhe mbunge wa jimbo la misungwi Charles Kitwanga,ambapo kila mwandishi amepewa shilingi laki mbili ili kutimiza lengo lake.lakini pia amemlazimisha (mtendaji wake wa mkoa) aambatane na wanahabari hao ili kwenda kuwachukua madiwani wachache ambao pia wamepewa hela ili wamzungumzie kitwanga kwa kumkejeli na kumtukana.
Tunaomba watanzania na waandishi wa habari mjue kwamba rais magufuli kwa sasa anavita kubwa na wasiomtakia mema na wanatumia mbinu mbalimbali kuhakikisha kuwa wale watu wote ambao wanamthamini na kumkubali anakosana nao.
Sisi madiwani wa misungwi tunasema hatuna ubaya na rais wetu,lakini pia hatuna ubaya na mbunge wetu na wote tunawapa ushirikiano kama kawaida na tunawaomba pia watanzania wote kwa dini zote kwa rika zote mpeni ushirikiano rais wetu ambaye ana upendo wa dhati na wananchi wa taifa hili.
Tunamshauri mwenyekiti wa ccm mkoa wa mwanza aachane na makundi baada ya mchakato wa urais kupitia ccm kumalizika tunajua alikuwa na mtu wake lakini kwa sasa rais ni mhe John pombe magufuli na tunamuomba antonny diallo akubali na ampe ushirikiano kwa asilimia mia moja.
(......) tunasikitika na tunawataka vyombo vya habari watende haki na watumie kalamu zao kwa kutenda haki kwa kila mtanzania awe maskini ama tajiri.
Imeandaliwa na Majumuisho IDDY mwananchi mzalendo kutoka Misungwi
Asanteni na Mungu awabariki

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 17/06/2016