Suala la Dkt Mengi latinga bungeni

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,369
Reaction score
27,785
Suala la Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, kutishiwa maisha na kutakiwa kwenda kuripoti polisi limezua mjadala bungeni, baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, kuitaka serikali kutoa ufafanuzi baada ya kutoa mfano wa mbunge mmoja kutishiwa maisha na Mwanasheria mkuu wa serikali, lakini alipokwenda kuripoti hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

Mbilinyi alitoa kauli hiyo wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya wizara hiyo, kuwa bunge lililopita Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, alitishiwa maisha na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, na pamoja na kutoa ripoti polisi hakuna hatua zilizochukuliwa.

Akichangia katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, mbilinyi alisema: “Nataka ufafanuzi tunamsaidiaje huyu mwenyekiti ambaye maisha yake yanatishiwa,” alisema.

Baada ya kauli hiyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alimtaka Mbunge kutochanganya mambo ya kisera na mshahara wa waziri na kumtaka kuegemea kwenye hoja iliyo mbele.

Aidha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Uratibu na Bunge), Jenister Mhagama, alisimama na kutoa ufafanuzi kuwa Mbunge ametumia lugha ya dhihaka dhidi ya rais na kulitumia katika kushawishi bunge kuamini katika jambo lililotokea.

Mhagama alisema si kweli kuwa rais ametishia maisha ya Mengi na kumtaka Spika Makinda, ambaye kwa wakati huo alikaa kama mwenyekiti kumtaka Mbilinyi afute kauli yake.

Hata hivyo, Mwenyekiti alisema suala hilo ni la jinai hivyo, halikubaliki kujadiliwa bungeni na kutaka bunge liendelee kupitisha vifungu vya bajeti ya wizara hiyo.

Awali akisoma maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani, Mbilinyi alisema kambi hiyo inalaani taarifa za kutishiwa maisha kwa mmiliki wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Dk. Mengi, kwa madai kuwa kituo chake kimekua kikitoa habari za kiuchochezi zinazosababisha kuyumba kwa serikali ikiwamo habari za kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya akaunti ya Tegeta Escrow.

Alisema sheria mpya ya habari inalenga kuminya haki ya Watanzania kupata takwimu sahihi ambazo zinaweza kutolewakwa usahih na wadu wengine ambao wanashiriki katika mchakato wa uchaguzi mkuu.

Alisema muendelezo wa malalamiko dhidi ya sheria hizo kandamizi pamoja na Muswada wa Habari ambao unaelezwa kuwa katika mkakati wa kuletwa ndani ya bunge hilo, umepingwa vikali pia na wadauwengi nchini kikiwamo Chama cha Wamilikiwa Vyombo vya Habari nchini (MOAT).

SOURCE: NIPASHE
 
Mliopo Arusha mtujuze naskia posho zimeanza kulipwa asb hii kwa ajili ya supu
 
Ukitishiwa maisha si unaenda kuripoti polisi kwa hatua zaidi za kijinai? Huyu Mzee amewageuza wabunge kuwa mavuvuzela ya kutanganza maslahi yake binafsi ndani ya chombo cha umma na mhimili muhimu wa dola ambacho kilitakiwa kujadili matatizo ya wananchi wote wa Tanzania.
 
kweli mnafaa kuwa milembe!
-hivi ni kweli mengi akaripoti policcm ambayo nayo ni sehemu ya rais kimamlaka ya kiuteuzi??


'mengi tutamtetea sisi wanyonge wa nchi hii na ole wao wamuuwe haki yanani wao na familia zao labda wakaishi chini ya bahari!!

--chama cha c.c.m kinataka kufa na watu muhimu kwa nchi yetu.
 
Kweli mzee kasema sana kuhusu jambo hilo la kutishiwa uhai wake
 
Hakuna mtu ambaye amewahi kushindana na mengi akashinda Manji+ Muhongo mfano hao wote wamedondokea pua
 
Mbilinyi Kichwa Jenesta anawayawaya tu hana maelezo kamili labda wamtafute mchongeaji ZZK
 

Gazeti la Mengi hili linamsaidia kumtetea!!Mwandishi wa story hii aje atuambie hapa kwa kuwa anafanya kazi kwa Mengi je ana mkataba wa ajira??
 
Mbilinyi Kichwa Jenesta anawayawaya tu hana maelezo kamili labda wamtafute mchongeaji ZZK

Mbilinyi mchumia tumbo tu kavuta mpunga kwa Mengi ili asimamie shoo ya kumtetea,Who is Mengi??anamiliki vyombo kibao vya habari na misaada kibao, angalia waandishi wa habari wanaofanya kazi kwenye makampuni yake wana shida hili halisemi anaogopa sheria itakayomlazimisha kuwakatia bima waandishi wake,kuwapa mikataba ya kazi ya kueleweka na kuacha kuajiri watu wasio na taaluma ya habari kwa manufaa yake binfsi,mnyonyaji tu huyo!,
 
hawawezi kukuelewa mkuu

Wewe ni miongoni mwa watu waliowekwa mfukoninna Mengi,anamiliki vyombo kibao vya habari na hivyohivyo anavitumia kueneza propaganda na porojo zake ili watanzania wamuamini, tena anapewa airtime kibao hata kama jambo lenyewe ni kujishitakia kwa wananchi eti katishiwa,ana vyombo sawa na alikua wa kwanza kupinga sheria nyingi tu ila hii ya HABARI kaona inaugusa moyonwake kaamua kuingia mzimamzima ili aendelee kuwanyonya waandishi wa Habari na kuua tasnia ya HABARI NCHINI.
 

Katishiwa wapi hata kovu hana,Protectionmechanism hiyo tumeshamzoea!!
 
Wewe acha kujidanganya mitandaoni ndugu. Wewe una ubavu wa kumtetea Mengi? Unamtetea dhidi ya nini? Hivi kweli kwa akili yako ya JF unamuona Mengi anafanana na mtu aliyetishiwa maisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…