STRANDED!msaada tafadhali



bora useme wewe....hakuna alienielewa naona
 
hata nilipokuwa msichana nilikuwa najua nataka nini kwenye maisha!
 
Wewe dada usirudie matapishi, nadhani wakati unateseka pengine ulimwomba mungu akusaidie kukupatie mtu ambae yuko serious, sasa umempata halafu unataka kurudi kwenye mateso. kumbuka methali isemayo ''mkataa pema pabaya pana mwita'' sasa kama huyu wa sasa hajakukosea kwanini ufikirie kumwacha na kumrudia yule aliyewahi kukutesa hapo nyuma? hapo utakuwa unajitafutia laana mwenyewe. TULIA KUWA NA MSIMAMO, NA UPENDO UTAZIDI KUONGEZEKA KWA HUYU ULIENAYE SASA: Ila ikiendelea kuwa na mawazo mengine ya kurudiana yatakusababishia kuyumbisha msimamo wako na hivyo upendo wako kwa huyu wa sasa utapoa maana unaweka mawazo mengine.

penda unapopendwa using'ang'ania usipopendwa labda kama hujipendi mweyewe. hiyo roho inayukurudisha nyuma kumfikiria yule wa zamani inakutafutia balaa na laana. Na ukifanya hivyo nuksi itakufuata na utachekwa na kila mtu.
 
Unampata mtu anakujali, anakuthamini na kukuonyesha mapenzi ya kweli halafu unataka kumpotezea!!! Acha upumbavu weye!!! Tuliza akili ufanye maamuzi yaliyo bora badala ya kurukaruka huku na kule.

 
Last edited by a moderator:
Mdogo wangu usiwe slave wa mapenzi.What makes u think your x has changed?
Hata kama ame change kwa kweli u can not justify kurudi kwenye mateso aliyokupa wakati u have a man who loves u.
Make wise decision sister
 
Kitendo cha kuleta mada kuomba ushauri humu kinaonesha upeo wako!!
Lets assume wengi wanakwambia umrudie, utarudi?! Ushasema uliyenaye ni by far anamzidi yule wa zamani, nini unachokitaka?!

Hujui unalotaka!!
Subiri dunia itakufundisha!
 
Oooh! Maskin dada wa watu usirud nyuma endelea na ulie nae huyo ex kaona msimamo wako anataka kukuumiza zaid, lengo lake alitaka kukufanya uwanja wa mazoez. Kuwa makin sana ukirudiana nae atakuja kukutenda kwa wakat ambao hutarajii na utakuja kujuta maisha yako yote hebu msahau kabisa huyo nyang'au
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…