Shishangai jimbo hilo au Wilaya hiyo ni ngome ya SSM!!! Kwa nini wasichoshwe Oktoba 2010?? Tangu SSM izaliwe na kushika hatamu, kwa nini wasibadilike maana yenyewe imeshindwa kuwabadilisha?? Kijiji nilichosomea sikuwahi kukaa chini kuanzia nursery school!! Nilipopata fursa ya kuja DSM (nikiwa bado mdogo nasoma kijijini-nilikuja kutembea kwa ndugu jamaa na marafiki, si unajua tena extendend family)!! Nilishangaa kuona madarasa DSM hayakuwa na madawati?? Japo pia nilishangaa maendeleo yake mengine ambayo hayakuwa kijijini kipindi kile (umeme). Nikashangaa wenyeji wangu maji yalikuwa ya shida wakati kijijini tulikuwa na chemichemi, mifereji na maji ya bomba!!! Kweli Tanzania tembea uione makuuu!!!