Serikali haina fedha za kujiendesha na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, sasa wameamua kukopa toka katika mifuko ya hifadhi ya jamii na wameshindwa kulipa. Wamekopa NSSF, PPF, PSPF na LAPF mabilioni ya fedha ambayo wameshindwa kuyalipa.
Kwahiyo njia pekee ya kujinusuru na aibu hiyo wakaona ni kwa kusitisha fao la kujitoa ili wajipange, kitu ambacho hakikubaliki hata kidogo kwetu sisi wanachama wa hiyo mifuko ya pensheni.