Star TV na RC Makonda: Kilichojiri katika mahojiano

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Watangazaji ni Leonard Mapuri na Aloyce Nyanda walioko Dar es Salaam na Samandu Hassan akiwa Studio za Mwanza
Swali: jina la Bashite ulikua unalijua mwanzo?
Makonda anasema jina la Albert Bashite kwa kifupi alipoanza madawa ya kulevya ndio amaeanza kusikia majina mengi na kashfa za kifamilia na mali
Ameulizwa Jina la Bashite amelianza kusikia kabla au baada ya vita ya madawa?
Makonda amesema swali hilo haliwezi kumsaidia yeye katika utendaji wake wala wananchi anaowaongoza

Pia yeye na mkewe wameandika changamoto zilizojitokeza baada ya kuanza mapambano na watatoa kitabu kuhusu hilo
Swali lingine ni aliposali makanisa mawili hadi kulia alitikiswa na skendo za Bashite?
Makonda amesema kusali kwake na imani yake haiathiriwi na watu na alienda kwa sababu alikuwa akitimiza mwaka mmoja kama mkuu wa mkoa na aliona aanze na Mungu

Mwandishi anamuuliza lakini ni kwa nini alilia? Makonda anasema ukiwa unajadili kitu lazima uwe ndani ya kitu chake na mtu anayeamini anajua mtu anaposali hisia anazopata wakati wa kusali na kuna watu walikuwa wanatuma mapepo kwake yakamgomea

Swali lingine: Alitaja majina ya watuhumiwa wa madawa kwa kisasi na kuna watu wake wa karibu wanauza hakuwataja?

Makonda anasema cha kwanza ni kuelezeakwa nini aliingia kwenye vita ya madawa ndio alitakiwa aulizwe kwanza, anasema alijifunza kwa miezi sita kuhusu biashara hiyo na kugundua kuna biashara za madawa yenye viwango vya juu na madawa yenye viwango vya chini.

Biashara hii inatesa familia nyingi na kufuta ndoto za vijana na yeye Mungu amampa nguvu za kupambana na wanaoua ndoto za vijana, pia ilani ya CCM inapinga matumizi ya madawa na pia sheria zilizotungwa na bunge zinapinga vikali matumiziya madawa

Anasema njia za kutaja majina ni kuwa alikuja nalo kwa kuwa lengo lake ni kupunguza madawa ya kulevya na sio kukakamata watu, ukitaka kukamata watu ndio utafanya kimyakimya.

Alipewa taarifa kutoka kwa wananchina vyombo vya serikali kuhusu wanaofanya biashara hiyo
Na walioitwa polisi ilikuwa ni priveledge kwao kwa kuwa iliwapa nafasi ya kujieleza na kujisafisha
Wapowatu waliojieleza na kukutwa na matatizo na wapo waliokiri wenyewe na kusaidiwa, wengine walikuwa hawajui maeneo yao yalikuwa yakifanyiwa biashara hiyo na wakaonyesha ushirikiano pia wapo wengi waliokamatwa bila kuitwa
Yoyote yule nayesema aliitwa kwa kisasi ajiulize alikosana na Makonda wapi na Makonda ni taasisi sio mtu.

Kwenye utumishi wa umma ana miaka 2 na miezi 4
Swali lingine ni katika vita alinufaika yeye binafsi kwa kutumia matajiri na gari alizonazo ni moja ya mali alizojinufaisha nazo ana nyumba za kifahari Mwanza ana mali kiasi gani?
Makonda anajibu hizo n moja ya tuhuma alizopata ila alikua anaanza maisha kabla ya kuwa mtumishi wa umma ana maisha kabla ya ukuu wa wilaya na mkoa
Na pia hilo sio kweli kuwa ana majumba na magari amewaalika waandishi wamtembelee nyumbani kwake na sio kila mali ataipata itakua ni ya kwake nyingine ni za umma
Kama kuna mtu wa madawa anakupa gari ili usimtaje halafu akupe gari wakati wanaohusika na kupambana ni serikali nzima na sio yeye atatokaje?
Na kuna ushahidi kuwa njia aliyoiytumia ya kutaja majina imepunguza madawa ya kulevya mtaani kuliko iliyokuwa ikitumika mwanzo
Swali :Tuhuma ya Makonda kuhusu vyeti na anatumia cheti feki na kuna mtu Tabora anaitwa Paul Makonda

Makonda anasema Historia yake ipo wazi sana na hajaibukia kwenye ukuu wa mkoa na maswali ya waandishi yatamsaidia wananchi kupata maji na huduma bora na kama kuna mtu anayetaka kujua kuhusu eleimu yake amfuate wizara husika

Swali: Kwa nini asitaje hadi wananchi waende kwa waziri husika na aliyemteua?
Makonda anasema kwa nini unataka leo wakati amenanza kitambo hadi aanze kupambana na madawa ? amesema hana muda wa kuzungumzia maswala ya vyeti kwa sasa kwani yalikuwa yameshaelezewa na yeye kitambo anataka maswali kuhusu maendeleo
Amesema ametajwa yeye ni shoga na hana uwezo wa kuzaa na hawezi kujibu kila linalotupwa kwake umuite Makonda au jina lingine yeye atapambana na madawa ya kulevya

Swali: Tunajua Wakuu wa mikoa hawahusiki na vyeti sisi tunajua huhusiki tunataka ukweli

Makonda anajibu ukweli ukiutaka nenda kwenye historia ya upamabanaji wa madawa ya kulevya, ukiwa kapteni ukipigwa na mawimbi hutakiwi kubadilisha uelekeo na kusema wafanyabiashara hawezi kumsimamisha

Swali jingine, Kuna watoto wa vigogo wanaotuhumiwa ukiwataja wengine ni rafiki zako

Makonda prediction sio mbaya ya mtu kuwepo lakini prediction inatokana na mazingira na walienda kwa hatua na waliona ni busara hatua waliyofikia ni bora wamkabidhi kamishna aendelee nayo, na mpaka wake ulikuwa ni mkoa wa Dar na kama kuna mtu unayemfahamu alikuwepo mfajhamishe na ataiwasilisha kwa kamishna.
Swali Mkoa wa Dar ulifanya vibaya matokeo ya kidato cha nne , na hukuzungumzia hilo ni kwa sababu ulikua kilaza na wewe?
Makonda anasema matokeo hayatengenezwi siku moja ni process na unaweza kuonekana ni kiongozi wa kauli ukiwa unatoa kauli kila kitu, elimu huanza darasa la kwanza. mtu mwenye akili huanza na procees ya elimu na sio matokeo

Aliamua wilaya zote zikae ni kwa nini walipata matokeo mabaya? na alipata majibu pia kwenye kikao cha RCC walizungumzia hilo na kutengeneza mkakati pamoja na wabunge wote wa Dar kutengeneza mkakati wa kuondoa hilo janga na sio kutoa kauli

Swali:Umekua ukitoa kauli kwenye mambo mengi ndio maana tumekuuliza hilo mfano ulisema waliomuonyesha rais mabango ungewachapa hilo si lilihitaji process pia?
Makonda anasema waandishi wamekua waki focus kwenye mabaya na hiyo kauli imekua na nguvu kuliko kilichozungumzwa, na kusema waandishi wasipomuuliza maswali kuhusu ardhi atawaona ni watu wa ajabu Makonda anaendelea kuzungumzia kero za ardhi
 
Makonda anayelelea idadi ya kilomita za barabara za Dar es Salaam, barabara zenye lami, zilizojengwa kwa changarawe na zile korofi
 
Naona makonda kawalipia nauli ya ndege hao watangazaji ambao inajulikana wazi kituo chao cha kazi ni mwanza,nadhani na posho ya kujikimu kawalipa kupitia GSM

Hongereni watangazaji wa startv Dar es salaam kwa kugomea kufanya mahojiano na Bashite mpaka imebidi hao wasafirishwe mpaka Dar
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom