Kosa kubwa alilofanya Sitta ni kutumia Uspika kujiandaa na kampeni za urais 2015. Alitaka kutumia vita dhidi ya ufisadi kama njia ya kumtengenezea mazingira mazuri kwa 2015. Naona mpango wake ume backfire vibaya mno.
Miongozi mwa makosa aliyofanya ni kuwapendelea baadhi ya wabunge kwenye maaumizi na hivyo kuwafanya wabunge wengine washutuke. Kibaya zaidi amekuwa akitumia pesa za umma kuwahonga baadhi ya wabunge kwa fadhila mbalimbali ambazo hawakustahili.
Huwezi kupigana na majambazi huku mwenyewe ni jambazi. Laiti kungelikuwa na chombo huru cha kuchunguza malipo yaliyofanywa na ofisi yake, wangegundua madudu mengi mno ambayo yalifanywa kwa endorsement ya mr Sitta mwenyewe.
Bunge lijalo asahau kabisa kuwa spika, atumie muda uliobaki ili angalau aweze kurudi bungeni. Naona bado hajatubu wizi aliotufanyia Watanzania alivyokuwa kwenye uendelezaji wa makao makuu Dodoma.