Spika Samwel Sitta atangaza kugombea tena uspika bunge lijalo

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,512
6,145
Nimetazama taarifa ya habari TBC1 nimepigwa na butwaa kusikia Spika Sitta anatangaza nia kugombea tena uspika...daaah kweli mzee kaanza kuogopa kivuli chake.
 
Nimetazama taarifa ya habari TBC1 nimepigwa na butwaa kusikia Spika Sitta anatangaza nia kugombea tena uspika...daaah kweli mzee kaanza kuogopa kivuli chake.

nyota inang'ara kwa anna makinda. mbaya zaidi hawaivi na NEC ya chama chake.........
 
nyota inang'ara kwa anna makinda. mbaya zaidi hawaivi na NEC ya chama chake.........

nimecheka kweli kumsikia Spika alivokuwa anaongea..hahaaaaaa standard and speed sifuri...eti next bunge atakuwa bora zaidi
 
nimecheka kweli kumsikia Spika alivokuwa anaongea..hahaaaaaa standard and speed sifuri...eti next bunge atakuwa bora zaidi
Hahaaa! Mkuu, kakiri udhaifu kwenye uongozi. Amekuwa muungwana!
 
yaani sita kawa mdogo kama punje ya ulezi..mwe kweli mafisadi wanatisha.toka watake kumpora kadi ya CCM kawa mtulivu sana
 
yaani sita kawa mdogo kama punje ya ulezi..mwe kweli mafisadi wanatisha.toka watake kumpora kadi ya CCM kawa mtulivu sana

........................pia mtandao wake wooooote wa waliojiita wanapinga ufisadi umesambaratishwa na kusahaulika ndani ya sekune tu.................. sasa ahesabu amefulia...........hapati hata unaibu spika!!!!! akibahatisha ubunge akatambike upya !!!!!!!!
 
Ni haki yake ya kikatiba ni vizuri wanaotaka ku -compete naye waweke nia zao ukifika muda muafaka
 
Hafwai hata kwa ubunge wa urambo achilia mbali uspika

afadhali ya Msekwa huyu hafai hata kuwa mwenyekiti wa kamati yoyote ya bunge.ana chuki na visasi na hana msimamo mwepesi wa kuomba msamaha anapoona kazidiwa...alikuwa na haja gani kuomba msamaha wakati wanataka kumvua uanachama?mbona sijawahi kusikia EL anatoa hata kauli ya kuomba kuimarishiwa ulinzi.hahaaaaa Sitta unachokoza ngumi wakati unaogopa kutolewa manundu
 
Sitta alionyesha udhaifu wake toka pale alipompinga Dr. Slaa na report ya Mafisadi halafu baadae akageuka na kujifanya yeye ndio kinara wa wapinga ufisadi!! Sasa maji yamemfika shingoni anatapatapa na kutangaza kuwa atawania uspika bunge lijalo, nani kamwambia atarudi mjengoni; kwani mafisadi wamekwisha mfanyia mahesabu ya kumuangusha na Kapuya ndio point man wao kule Urambo!! Sitta jinsi alivyoliendesha bunge juzi na kufunga mjadala wa RICHMONDULI imemshushia heshima mbele ya macho ya wadanganyika walioamini kuwa aliku mpiganaji wa kweli!!! Huo uspika anaouota wenzie wamemuandaa auchuke ALIKWINA!! Kama hamumjui waulizeni wabena wa Njombe.
 
Kwani Sam Six ana umri gani?Age is nothing,ila utendaji wake sio mzuri kabisa.
Anyway yuko sawa na akina Msekwa,wako kwa manufaa binafsi.
 
Is he real serious au anatutania? Hiyo miaka aliyokuwa hapo hana lolote la maendeleo ambalo amefanya. Umri umri unagomba mzee kahimize kilimo kwanza kijijini kwenu kulikoni
By the way who is 'ALIKWINA' ? Bulesi tafadhali naomba unijuze mimi ni mbena mbona simjui huyu mtu au ana jina lingine? Tafadhali naomba msaada wako.
 
Nyie nafikiri hamuijui CCM mbali ya utendaji mnaousema mbovu six atarudi mjengoni tena kwa kura nyingi tu na u spika anaupata mtashangaa
 
sam six kuupata uspika ni kama ngamia kupenya katika tundu la sindano, hawezi kuupata tena unless amuombe msamaha EL na wenzake, hata hivo ni ngumu sana kumwamini kwa sasa!
 
Kosa kubwa alilofanya Sitta ni kutumia Uspika kujiandaa na kampeni za urais 2015. Alitaka kutumia vita dhidi ya ufisadi kama njia ya kumtengenezea mazingira mazuri kwa 2015. Naona mpango wake ume backfire vibaya mno.

Miongozi mwa makosa aliyofanya ni kuwapendelea baadhi ya wabunge kwenye maaumizi na hivyo kuwafanya wabunge wengine washutuke. Kibaya zaidi amekuwa akitumia pesa za umma kuwahonga baadhi ya wabunge kwa fadhila mbalimbali ambazo hawakustahili.

Huwezi kupigana na majambazi huku mwenyewe ni jambazi. Laiti kungelikuwa na chombo huru cha kuchunguza malipo yaliyofanywa na ofisi yake, wangegundua madudu mengi mno ambayo yalifanywa kwa endorsement ya mr Sitta mwenyewe.

Bunge lijalo asahau kabisa kuwa spika, atumie muda uliobaki ili angalau aweze kurudi bungeni. Naona bado hajatubu wizi aliotufanyia Watanzania alivyokuwa kwenye uendelezaji wa makao makuu Dodoma.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom