Spika Job Ndugai anatamani "pepo" lakini hataki "kuokoka"

mwankuga

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
336
225
JOB NDUGAI ANATAMANI “PEPO” LAKINI HATAKI “KUOKOKA”.

Niliandika, naandika na nitaandika daima. Ndio, napenda kuandika. Tarehe 7 Machi, 2011 niliandika makala moja yenye kichwa “Hizi ndizo sifa za kiongozi bora”. Katika makala hiyo nilijaribu kuanisha matatizo ambayo Afrika inakumbana nayo, ambayo kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na viongozi wabovu. Nanukuu baadhi ya maandishi ya kwenye makala hiyo:

“Moja kati ya sifa za ndani za kiongozi bora ni kama vile, to be fair (not favour or fear), tabia njema ,mpenda amani, mtulivu, mwaminifu ,mwenye busara, anayependa kusaidia watu, si mbaguzi, mchapakazi, anayeweza kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati, mtu wa wote, asiyemilikiwa na kikundi chochote, awe na uwezo wa kuwasiliana na watu anaowaongoza, awe tayari kusikiliza pande zote za hadithi kabla hajatoa maamuzi, mkweli na muwazi, asiyehukumu bila ushahidi, awe tayari kukosolewa, awe mcha Mungu n.k”

Aidha nilieleza kwamba ni rahisi sana kuwakosoa viongozi wa namna hiyo, lakini kazi ngumu zaidi ni namna ya kuwapata viongozi bora. Kwa namna ambavyo mifumo yetu ilivyo ya kuwapata viongozi ,si ajabu sana kupata viongozi “vilaza”. Viongozi wengi wa kisiasa hupatikana kwa njia ya uchaguzi, lakini hakuna mtu asiyejua kwamba chaguzi nyingi za Afrika, anayeamua nani ashinde sio mpiga kura, bali anayehesabu na kutangaza matokeo.

Tarehe 5, Juni 2016 niliandika makala nyingine yenye kichwa “Uongozi wa Bunge Umepwaya, ujitathimini”. Niliandika makala hiyo kutokana na hali iliyokuwa inaendelea bungeni chini ya uongozi wa Spika Job Ndugai, na Naibu Spika Dr. Tulia Mwasasu. Nilihitimisha kwa kusemaUongozi wa bunge unatakiwa kujitathimini kama unaenda sawa. Nafasi ya kurudi kwenye mstari bado ipo. Ili bunge liweze kuisaidia serikali, sio kufunika na kuzuia hoja na mijadala yenye masilahi kwa taifa, bali kuacha bunge kutimiza majukumu yake. Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema "bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambacho kitakuwa na madaraka kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba hii".

Tangu niandike makala hiyo, kuna matukio mengi ambayo yametokea, huku bunge likiendelea kuwa tawi la serikali. Niliamini kwamba Job Ndugai ,kwa uzoefu wake na uendeshaji wa bunge pengine angebadilisha hali ya mambo. Sikuwa na matumaini yoyote kutoka kwa dada yangu, Tulia Mwansasu, maana yeye ana “kazi maalum”.

Kilichonifanya kukumbuka makala za nyuma na kuandika makala hii, ni mambo yaliyotokea bunge juma lililopita, ambapo wabunge wawili wa Chadema Esther Bulaya na Halima Mdee kuambiwa wasikanyage bungeni hadi mwezi wa nne, 2018. Tatizo langu si yale ambayo wabunge hao walifanya, tatizo langu ni namna Ndugai alivyofura. Ndugai aliamua kuonyesha sura na tabia yake halisi ambayo haionyeshi taswira nzuri kwa uongozi. Wakati wa kampeni za uchaguzi wa ubunge ndani ya CCM, Ndugai alidaiwa kumpiga fimbo mgombea mwenzake. Kumbe hii ni tabia yake.

Alipowaamuru askari wa bunge, kumtoa John Mnyika ,Job Ndugai alionyesha jinsi alivyo na hasira na ubabe usio na maana. Kwa maoni yangu ,askari hao walitii amri ya spika, lakini walitumia utu sana. Lakini Job Ndugai sijui alitaka askari hao wamfanye nini John Mnyika. Kitendo cha kuwafokea na baadaye kutangaza uamuzi wa kuwatoa askari hao kulinda bungeni, ilikuwa ni wazi kwamba Job Ndugai hafai kuwa kiongozi wa umma, achilia mbali kuwa mkuu moja ya mhimili muhimu.

Ni Ndugai huyu ambaye anataka siku moja wananchi waje kumkumbuka kwa utendaji uliotukuka. Ndugai anapenda apate sifa nzuri, lakini hataki kufanya yaliyomema. Kwa kipindi hiki cha utawala wa awamu ya tano, Ndugai alitakiwa kuwa imara sana, na kulifanya bunge kuisimamia serikali ipasavyo. Kwa bahati mbaya sana, ndani ya kipindi kifupi sana, Job Ndugai ameonekana kushindwa kuhimili vishindo vya serikali, na kukifanya chombo hicho kama jumba la kuonyeshea “sinema”. Bunge limegawanyika vipande vipande. Mambo ya msingi yote hujadiliwa kwa misingi ya vyama, lakini mambo ya hovyo wabunge huungana. Katika mazingira kama haya, Job Ndugai angeweza kuwa shujaa kwa angalau kusimamia kanuni za bunge na kuisimamia serikali angalau kwa asilimia 50 tu. Pamoja na kwamba Marehemu Samwel Sitta kuwa na mapungufu yake, lakini kuna mambo muhimu kwa taifa aliyasimamia.

Ndugai anatamai “pepo” lakini hayuko tayari “kuokoka”. Ili Job Ndugai apate utukufu lazima akubali kubadilika. Kwanza lazima ajitahidi kujizuia na zile hasira zake kama alivyompiga bakora mwenzie na kuwafokea askari bungeni. Pili, ajaribu kusimamia kanuni za bunge kwa usawa, bila kujali zinamfurahisha au kumchukiza nani. Akiamua kuweka masilahi ya Taifa mbele atakumbukwa daima, lakini akitanguliza hasira zake na masilahi ya chama chake, atawekwa kwenye vitabu vya kumbukumbu ya viongozi wa hovyo kuwahi kutokea katika taifa letu.

EM kutoka kijijini Lupata.
 

Mbojo

JF-Expert Member
May 31, 2011
1,408
2,000
Hawa hata malaika ashuke hawawezi kumwelewa. Leo chadema wamekuwa mafisadi! Hivi wanaoteketeza mali za Nchi hii ni chadema! Hata kwa mimi nisiye na chama siwezi fikiri ovyo namna hii.
 

mommythebest

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
516
1,000
The man acted as if he will forever be the Speaker. It's as if kamwe yeye haitotokea aje kuwa mbunge wa kawaida potelea mbali kuwa mpinzani. Sijawahi muombea mtu mabaya wala i have never hated anyone , lakini may God forgive me kwa vile nawafikiria watu wa dizaini ya huyu mgogo na wenzake. Laana na iwe juu yao kwa uonevu wanaoufanya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom