South Africa declared 5 days of mourning for Nyerere!

K.Msese

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
2,385
3,012
Africa ya Kusini ilitangaza siku (5) tano za maombelezo ambapo bendera zilipepea nusu mlingoti! Tumuunge mkono Jk kwa maombelezo ya siku tatu ya nchi yetu juu ya kifo cha Madiba!

....If Mwalimu Julius Nyerere had been the founding father of South Africa and not Tanzania, he would hardly have received a more dignified farewell here than he has done.
 
Hao na walimwengu wengine ndiyo wanaomjua Mwalimu. Hapa mkianza kumjadili mnamtukana kana kwamba hakuna lolote wala chochote kwa ustawi wa ulimwengu huu. Mwalimu ni Mwalimu wa ukweli. Alipendwa na kuthaminiwa kutokana na maono yake ya kuwatetea wanyonge. Vijana wa Tanzania wamezama kwenye Bongo Movie na Bongo Fleva, hawajui watu muhimu kama hawa. Sana sana kwao John Cina ni wa maana na muhimu kwao kuliko wazee kama Mwalimu, Madiba, Samora, Kwame, Sankor, Kaunda na wengine wengi.
 
Hizo ni rambirambi zao wakati amekufa, ulitegemea wakati wa maombolezo ya kifo chake wazungumzie nini zaidi ya maneno ya kuwafariji watu wake?

Yaliyozungumzwa wakati wa kifo chake yachukulie kuwa ni maneno ya kuwafariji watu wake katika kipindi kigumu cha msiba.
 
...kuna watu walibeza juu ya Tanzania kuomboleza kifo cha Mandela (RIP) kwa siku tatu...kana kwamba wao (RSA) hawakuomboleza wakati wa kifo cha Julius Nyerere!..kwamba ni kujipnd tu....kwa JK!
 
Kwenye maombolezo haya, hapa Tanzania, ofisi za serikali zitafunguliwa kama kawaida?
 
^^
Hawa walikuwa marafiki waliopatana! Hata kama hatuna ujasiri wa kuyafuata waliyoyaacha basi hata hilo la siku 3 lisitushinde
^^
 
Kwenye maombolezo haya, hapa Tanzania, ofisi za serikali zitafunguliwa kama kawaida?


Hivi mkuu ina maana hujui maombolezo ya kitaifa yanakuwagaje? In short ni kwamba bendera zinapepea nusu mlingoti, mzigo ni kama kawaida. Sharti lingine, masuala ya starehe yanatakiwa kudhibitiwa; kwa mfano kumbi za starehe marufuku kuendekeza starehe zilizopindukia, n.k. Lakini kazini ni kama kawaida kwani kufanya kazi nayo ni sehemu ya kumuenzi marehemu.
 

Mwalimu anatukanwa katika Awamu hii ya nne, ushahidi upo wa wapi matusi yaha yanapoanzia japo ni kwa sababu za kishenzi.
 

Lazima tukubali Mwalimu alikuwa na pande mbili kama wat wengine, so usishagae wtu wakikosa sana sana leo na kesho watu wakasifia sana sana.
 
Kati ya watu ambao hata kama kimwili hawapo pamoja na sisi lakini wanaendelea kuishi ni Mwalimu na Madiba. Wapo wengine pia lakini hawa ni mifano ya haraka sana!

Hawa waliamini kwenye falsafa ya "Living Today for Tomorrow"! Walipojifikiria wao walifikiria na ustawi wa binadamu wengine pia.

Nasikitika kuona kuwa watu wa kariba hili siku hizi hawapo popote na waliopo hawapewi fursa zozote zile!

Tumeendekeza umimi, ubaguzi, kujilimbikizia mali, utajiri wa haraka haraka kwa gharama/mbinu zozote na matendo mengine maovu huku tukiendelea kuzaliana! Laiti tungejua kuwa siku zetu za baadaye zitakuwa za kulia na kusaga meno kutokana na misingi ya kinyang'au tunayoijenga leo!

Mimi ni mwanafunzi wa maisha ya Nyerere na Madiba. Ninapotafakari maisha ya hawa ndugu zetu naona kwamba walikuwa binadamu zaidi ya watu wengi tulionao duniani.
Walikuwa na madhaifu yao lakini hayawezi kamwe kulinganishwa na mazuri waliyoifanyia dunia.

Ingependeza kama kila mtu akutane na moyo wake;kutoka humo aone ni jinsi gani anashiriki kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri/salama ya kuishi leo na kesho! Living Today for Tomorrow!

Ee MUNGU naomba utuinulie akina Nyerere na Madiba wengine...!
 
Mwalimu anatukanwa katika Awamu hii ya nne, ushahidi upo wa wapi matusi yaha yanapoanzia japo ni kwa sababu za kishenzi.

Kweli mkuu,watu ambao sio waadilifu wanamwogopa Mwalimu,maadili ya uongozi yamedidimia kabisa awamu hii ya nne.
 
Thabo Mbeki ilikuwa si tu mchango wa Nyerere ktk ukombozi wa S.Afrika,bali mchango wa Nyerere kwa maisha binafsi ya Thabo Mbeki.
Mwaka 2007 nilihudhuria mdaharo wa Mbeki ktk ukumbi wa Nkurumah,siku ambayo Mbeki aliwashangaa Watanzania kwanini Tanzanite inazalishwa Tz lkn A.Kusini ktk soko la Dunia ndio wanaongoza kwa uuzaji,akashangaa kwanini wanampokea kwa mbwembwe wakati yeye hapa ni kama nyumbani.
Thabo akasimulia akasema,miaka ya sabini alikuwa anatoroka S.Afrika kupitia S.Rhodesia,bahati mbaya akakamatwa,na sbb pale alikuwepo Ian Smith swaiba wa makaburu, wakawa wanamrudisha S.Afrika.....Zuma Jacob akiwa Mozambique exile,Nyerere alimtumia ujumbe Smith akamwambia Mbeki aachiwe mana ni raia wake,kwa kutumia majasusi wake Mwalimu akampenyezea Mbeki passport ya ”uraia“ wa Tanzania,ijionyesha Mbeki kazaliwa Nachingwea,Mbeki akatoka kupitia Tanzania akaenda UK...na ktk safari zake mpaka miaka ya tisini alikuwa akitumia passport ya Tanzania,hali iliyomsaidia kuendesha harakati za kupinga ubaguzi kwa urahisi...na akasema ajabu ni kuwa jina la kwenye passport lilikuwa la ”kimakonde“...hata walipomkamata wakijua ni Mbeki,passport yake ilionyesha hina kinyume,na ikamtambulisha kama raia wa Tz.
Kwa mtindo huu,ilikuwa ni sahihi kwa Mbeki kutangaza siku tano,maana zaidi ya Nyerere kuwa Rais wa Tz,lkn kwa Mbeki alikuwa ni baba,mshauri na mentor wake....
 
Sijui tutafanya nii walau tuwe hata na theluthi tu ya moyo wa hawa waasisi. Kimeibuka kizazi cha watu wenye tamaa ya mali bila kutumia njia halali na kujaa ubinafsi na kiburi. Mungu atusaidie
 
Aise inapokuja mijadala inayomhusu mwalimu huwa naingia woga kupitia comments.....tangu nikutanage na post za wanaopenda kuponda tuuuu........na wapondaji hao ukisoma comments zao, wanaonekana kabisa wana ufahamu finyu wa historia......matokeo yake huishia kuporomosha matusi.

Mpaka kuna wakati huwa najiuliza....kama mtu anathubutu kumuita mwalimu mbaguzi......ni binadamu gani basi duniani atakuwa na sifa za kuonekana sio mbaguzi.

Aliimba Marijani Rajabu.........KILA MTENDA WEMA ATAKUMBUKWA KWA WEMA.

Kama kuna makosa ya kibinadamu.....yatakuwepo tu kwani sie ni hao binaadamu, sio MUNGU.

Walale pema peponi Mwalimu na mzee Madiba.
 
Mpaka kuna wakati huwa najiuliza....kama mtu anathubutu kumuita mwalimu mbaguzi......ni binadamu gani basi duniani atakuwa na sifa za kuonekana sio mbaguzi.
Tupatie tafsiri ya neno Ubaguzi halafu tuangalie kama wanaomuita nyerere ni mbaguzi wapo sahihi au la.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…