South Africa Au Botswana

MfalmewaKiha

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
1,191
1,237
Ndugu zangu habari za majukum
Mimi ni kijana mwenye Elim ya kidato cha 6, Nim Tanzania, nina miaka 32 sina mke, sina mchumba. Siku /wiki chache Niliona Uzi ambao uliletwa na ndugu mmoja ambae ID yake hum Jf alifahamika kwa Jina la SHIBEKIJIJINI ambae kwa sasa ameamua kwenda SA kutafuta maisha, na kweli kafika SA,
ILa comment nyingi hum zilionyesha SA sio mahari salama kiutafutaji, japo wapo watanzania wenzetu wamefanikiwa kutusua huko na wengine wakiisoma Namba.

Sasa na mimi nimetamani kutoka nje ya Tanzania ili nikajaribu njee ya nchi hasa km SA au Botswana, wadau nisaidieni niende wapi ambako naweza kufanikiwa kupata kibarua chochote halali kwa wepesi kati ya hizi nchi mbili. Asante. Naomba kuwakilisha hoja.
Matusi, kejeri sio lazima sana.
 
Kwa elimu uliyo nayo we bakia tu Tanzania,sikukatishi tamaa ila utajutia ukienda huko...
Unaweza kujikuta unaingia kwenye mkumbo wa kubeba ngada(unga) au kupush ngada mitaani kitu ambacho sio kizuri!..
Binafsi sijawahi kufika kujionea reality ila katika kupitia mitandao tofauti na kusoma comments za watu walioko kule na wengine wanatoa ushuhuda,mdogo wangu chekecha akili yako kwanza usikurupuke...
Ila kuna baadhi ya fani kama fundi magari,udaktari,nurse hapo unaweza kutoka kwa maana ajira zake ni nyingi na wanahitajika kila siku kama ukiwa umetimiza vigezo na masharti.
Ukienda na hiyo form six yako kazi kubwa jiandae na kuosha vyombo restaurant,kuosha magari,nk....ukishindwa kuzivumili plus njaa yako basi u r likely to be drug pusher
 
Nenda tu mkuu kapambane maisha ni popote.

Anzia Botswana ukiona magumashi unasonga kwa madiba kwan sh'ngapi?
 
Kasomee ufundi wa kutengeneza magari na udereva kisha uende huko South na Botswana. Elimu ya kidato cha 6 haina msaada kwenye maisha haya bora Uwe na elimu ya darasa la 7 lakini una fani kuliko kuwa kidato cha 6 ambaye ni unskilled labour
 
Kwa elimu ya form 6 na bado unataka kujilipua
Na darasa 7 LA jE?

Fursa bongo ziko nyingi tu

Msimu was kilimo huu Ingia shamba kalime magimbi utatoboa tu maisha hayaitaji haraka

Nje ya inchi ya kugumu kila sehemu RAIA wamekaba
 
Attachments

  • Screenshot_2017-03-08-11-31-24.png
    Screenshot_2017-03-08-11-31-24.png
    467.1 KB · Views: 60
Kwa elimu ya form 6 na bado unataka kujilipua
Na darasa 7 LA jE?

Fursa bongo ziko nyingi tu

Msimu was kilimo huu Ingia shamba kalime magimbi utatoboa tu maisha hayaitaji haraka

Nje ya inchi ya kugumu kila sehemu RAIA wamekaba
Jamani
 
Ndugu zangu habari za majukum
Mimi ni kijana mwenye Elim ya kidato cha 6, Nim Tanzania, nina miaka 32 sina mke, sina mchumba. Siku /wiki chache Niliona Uzi ambao uliletwa na ndugu mmoja ambae ID yake hum Jf alifahamika kwa Jina la SHIBEKIJIJINI ambae kwa sasa ameamua kwenda SA kutafuta maisha, na kweli kafika SA,
ILa comment nyingi hum zilionyesha SA sio mahari salama kiutafutaji, japo wapo watanzania wenzetu wamefanikiwa kutusua huko na wengine wakiisoma Namba.

Sasa na mimi nimetamani kutoka nje ya Tanzania ili nikajaribu njee ya nchi hasa km SA au Botswana, wadau nisaidieni niende wapi ambako naweza kufanikiwa kupata kibarua chochote halali kwa wepesi kati ya hizi nchi mbili. Asante. Naomba kuwakilisha hoja. Matusi, kejeri sio lazima sana.

Ushauri wangu ni kuwa elimu ya kidato cha sita isikufanye usijaribu kufanya vitu vingine, ila kama unataka kwenda Botswana, nakushauri jifunze mambo ya saloon, kwa wanawake pia wanaume, hii itakusaidia kujua namna ya matumizi ya vipodozi mambalimbali na namna ya kuwapendezesha wateja wako. Mafundi ujenzi, mafundi seremala, wananafasi nzuri pia ya kupata kitu cha kufanya nchi kama Botswana na hii ni kutokana na ukweli kuwa wengi wamesoma na hawapendi kufanya kazi za kawaida.
 
Back
Top Bottom